MTOTO AUAWA KISA KUJISAIDIA BILA KUJISAFISHA ENEO LA MSHIKAMANO MANISPAA YA SHINYANGANB..SIYO PICHA YA MTOTOALIYEUAWA

Ni Siku chache tu baada ya mtoto kubakwa ,kuuawa kisha mwili wake kuwekwa kwenye boksi na kutupwa karibu na dampo la taka eneo la Ngokolo Mitumbani katika manispaa ya shinyanga,.
mtoto Jamila Ramadhani mwenye umri wa miaka minne ameuawa kikatili kwa kupigwa na fimbo na kipande cha bomba la maji cha plastiki kichwani  na mama wa kambo aitwaye Moshi Kasema mwenye umri wa miaka 35 aliyekuwa anaishi naye katika eneo la Mshikamano katika manispaa ya shinyanga kisha kukimbia kusikojulikana.
Kwa mujibu wa kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga kamishina msaidizi wa polisi Evarist Mangalla tukio hilo limetokea  jana  majira ya saa kumi na mbili  na dakika 37  na kuataja chanzo cha tukio hilo kuwa ni mtoto Jamila Ramadhani kujisaidia bila kujisafisha

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post