MBUNGE AZZA HILAL AONGOZA MAMIA YA WATU MAZISHI YA MHITIMU WA UDOM ZUHURA MASHAKA


Marehemu zuhura mashaka mhitimu wa UDOM enzi za uhai wake

Padre Emmanuel Makolo wa Parokia ya Busanda akiongoza ibada ya mzishi nyumbani kwao na marehemu


-Kushoto ni Richard Kabega akiwa na Said Nassoro wahitimu wa mwaka 2005 katika shule ya sekondari Kituli wakiwa eneo la msiba.

Baba wa marehemu Mzee Mashaka akiwa na mke wake wakiweka shada la maua katika nyumba ya marehemu

Walimu wa shule ya msingi Kituli wakiweka shada la maua

Walimu wa shule ya sekondari Kituli baada ya kuweka shada la maua

Wanafunzi waliosoma na marehemu katika shule ya sekondari kituli baada ya kuweka shada la maua


mheshimiwa Azza Hilal mbunge wa viti maalum jimbo la solwa akizungumza mara baada ya mazishi ambapo alisema Zuhura alikuwa kijana mwenye uwezo mkubwa darasani ambapo takwimu zinaonesha kuwa ndio msichana wa kwanza kupata daraja la kwanza katika shule ya sekondari kituli tangu ianzishwe mwaka 1997,na kuongeza kuwa kifo chake ni pigo kubwa sio tu kwa familia bali taifa kwa ujumla

Zuhura Mashaka alizaliwa katika kijiji cha Kituli wilaya ya shinyanga  mwaka 1990 akasoma katika shule ya Msingi na shule ya sekondari Kituli zilizopo katika kijiji hicho, mnamo mwaka  2008 hadi 2010 akajiunga na shule ya sekondari Nganza iliyopo mkoani  Mwanza kwa masomo ya kidato cha tano na sita,na baadae  kujiunga na Chuo kikuu cha Dodoma na kuhitimu Juni 28  mwaka huu akiwa na shahada ya elimu ya miamba madini(Geology).

Baada ya kumaliza masomo yake  alikwenda nyumbani kwao Kituli Julai 5 mwaka huu,na mnamo Julai 13 alisafiri kwenda mkoani Geita kutafuta kazi katika mgodi wa madini wa Geita(GGM) na kufikia nyumbani kwa kaka yake anayeishi mkoani humo.

Akiwa kwa kaka yake siku iliyofuata tarehe 14 Julai ghafla alianguka na kuanza kutoa mapovu mdomoni kisha kukimbizwa hospitali ambapo muda mchache tu akaaga dunia.


.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments