KUUCHUNA....!!! WANAUME WANAACHIKA NA KUNYIMWA TENDO LA NDOA

 

 
 Baadhi ya wanaume katika jamii wanakabiliwa na tatizo la unyanyasaji wa kijinsia kutokana na uoga,aibu na hofu ya kuonekana wanyonge kama jamii itafahamu changamoto hiyo katika familia yake, ikwemo kuachika bila sababu za msingi na kunyimwa tendo la ndoa na wake zao.
 
Afisa Ustawi wa Jamii mkoa wa Shinyanga,bwana Songelaeli Daniel ameiambia blog hii kuwa  sio wanawake pekee wanaonyanyasika kijinsia, bali pia kuna baadhi ya wanaumme ambao wamekuwa wakinyanyasika kutokana na uoga na aibu ya kuonekana hawafai katika jamii hivyo hulazimika kukaa kimya.
 
Alisema hivi sasa kuna mwamko mkubwa kwa wanawake mkoani humo kuhusu mambo ya kijinsia tofauti na siku za nyuma,ambapo sasa wanawake wanafika kwa wingi katika ofisi hizo kueleza shida zao,
,lakini wanaumme ni mara chache sana wakati wapo baadhi yao wanaachika bila sababu za msingi na wengine kunyimwa unyumba.
 
Katibu Mkuu wa Chama cha Kutetea Haki za Wanaume Tanzania(TAMRA),bwana Anthony Sollo amesema wanaume wananyanyasika kijinsia kutokana na imani iliyojengeka katika jamii kuwa mwanamme ndio kichwa cha familia hivyo kuongea mbele ya jamii kuwa wananyanyaswa  hufikiri kuwa ni kitendo cha ajabu na  kwamba wataonekana wako chini ya wanawake kitendo ambacho huona kama wataonekana wanyonge na kuchekwa na jamii inayowazunguka.
 
Amesema wanaume wanatakiwa sasa  kukitumia chama cha wanaume Tanzania kuhakikisha kuwa wanapata haki zao za msingi ikiwemo kusikilizwa katika vyombo mbalimbali vya maamuzi kama vile mahakama,jeshi la polisi na mabaraza mbalimbali yanayohusika na usuluhishi wa mambo ya ndoa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments