Watu wasiojulikana
wanaodhaniwa kwa ni majambazi wakiwa na mawe na mapanga wameteka magari mawili likiwemo
basi la Nkamba’s kisha kupora fedha na
simu za abiria na kujeruhi sita usiku wa kuamkia leo katika
barabara ya Shinyanga -Mwanza.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Evarist Mangalla
amesema tukio hilo limetokea leo saa sita
usiku katika daraja la 54 katika kijiji
cha Buchambi kata ya Mwadui-Luhumbo
wilayani Kishapu.
Magari yaliyotekwa kuwa ni pamoja na Basi la kampuni ya Nkamba’s lenye
namba za usajili T610 ARR scania pamoja na gari lenye namba za usajili T722 CKZ
aina ya Fuso ,yote yakitokea jijini Dar es
salaam kuelekea jijini Mwanza.
katika tukio hilo
abiria wameporwa simu na fedha ambazo hazijajulikana idadi wala thamani
yake.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527
Post a Comment