MAFUNZO KWA WAENDELEZAJI WA NISHATI YA UMEME VIJIJINI YAINGIA SIKU YA TATU KATIKA UKUMBI WA NEDMAN HOTEL MJINI SHINYANGA YAKIWA YAMEANDALIWA NA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI

 Awali wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya umeme nuru kwa washiriki,huyu ni Wakala wa Nishati Vijijini (REA)mtaalam Mshauri Mzumbe Musa akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi hapo juzi
 Mkuu wa wilaya akizindua mafunzo kwa waendelezaji wa nishati vijijini ambapo alisema uzoefu unaonesha kuwa waendelezaji wa nishati vijijini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa mitaji,utaalamu mdogo wa kiufundi na ugumu wa kupata mikopo kwenye benki za kibiashara na riba kubwa zinazoambata na mikopo hiyo
 Kushoto ni Wakala wa Nishati Vijijini ,ambaye ni mkufunzi katika mafuzo hayo akifuatilia hotuba ya ufunguzi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi
 Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akifuatilia hotuba ya mkuu wa wilaya
 Hotuba inaendelea katika ukumbi wa Nedman Hotel mjini Shinyanga
 Kulia ni Bwana Monga Paschal Edward ,akiwa na washiriki wengine akifuatilia hotuba ya mkuu wa wilaya
Picha ya pamoja ya washiriki na mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga.
 
 
Pamoja na kuwepo kwa sera ya taifa ya nishati inayolenga katika upatikanaji wa nishati bora kwa lengo la kukuza uzalishaji mali na kuendeleza huduma za jamii,uzoefu umeonesha kuwa waendelezaji wa nishati vijijini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi kama vile ukosefu wa mitaji,utaalamu mdogo wa kiufundi na ugumu wa kupata mikopo kwenye benki za kibiashara na riba kubwa zinazoambata na mikopo hiyo.
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Shinyanga Annarose Nyamubi wakati akifungua mafunzo ya umeme nuru katika ukumbi wa Nedman Hotel mjini Shinyanga  yaliyoandaliwa na wakala wa nishati vijijini ambapo washiriki wapatao 16 kutoka maeneo mbali mbali nchini,wanashiriki mafunzo hayo yatakayodumu kwa muda siku 9 kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kufunga umeme na mitambo katika maeneo ya vijijjini.
Alizitaja changamoto zingine kuwa ni uharibifu wa mazingira pamoja na waendelezaji hao wa nishati vijijini kutojua au kutokuwa na uhakika wa fursa mbalimbali zilizopo katika uwezeshaji wa kuanzisha na kusimamia miradi ya nishati vijijini.
 Hata hivyo bi Nyamubi alisema  wadau wa nishati vijijini wanaweza kukabiliana na changamoto hizo kwa kushirikiana na wakala wa nishati vijijini na taasisi zingine za mambo ya nishati na mazingira zilizopo ndani na nje ya nchi huku akiongeza kuwa mafunzo hayo yatasaidia katika kutoa mwanga zaidi juu y fursa zilizopo katika kupata ruzuku na mikopo yenye riba na masharti nafuu itakayowezesha kuwekeza katika sekta ya nishati na taarifa juu ya taasisi wanazoweza kuashirikiana nazo ili kuondoa changamoto hizo
Kwa upande wake wakala wa nishati vijijini,ambaye ni mtaalamu mshauri bwana Mzumbe Musa alisema kuwa mafunzo hayo yatakayodumu kwa muda wa siku 9 yanalenga kuendeleza miradi ya umeme nuru vijijini ambapo washiriki watajifunza kwa vitendo na nadharia namna ya kufunga umeme na mitambo.
“Tayari tumewajengea uwezo katika maeneo mbalimbali nchini mfano huko Iramba na Mkuranga lakini hapa Shinyanga pamoja na mambo mengine washiriki wa mafunzo haya watashiriki katika zoezi la kufunga umeme katika shule ya sekondari Mwamalili iliyopo ndani ya manispaa ya Shinyanga”,alisema Musa.
Bwana Musa aliongeza kuwa wakala wa nishati vijijini wameandaa mafunzo hayo ili kuwajengea uwezo washiriki hao ambao wamepatikana kwa njia ya matangazo kwenye vyombo vya habari kisha kutuma maombi ya kupatiwa mafunzo hayo wakiwa kama sehemu ya wadau muhimu sambamba na kuhamasisha matumizi ya nishati bora hasa katika maeneo ya vijijini lakini pia kama njia ya kupata ajira.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments