BASI LA SAIBABA LAGONGA TRENI MAJERUHI 24, WALIOBAKI HOSPITALINI HADI SASA NI 6

Monica Kabati  kutoka musoma mmoja wa majeruhi ambaye bado yupo katika moja ya wodi katika hospitali ya mkoa

Treni ikiwa imehama kwenye njia yake

Basi la saibaba likiwa limepasuka taili baada ya kuburuzwa umbali wa mita 30

Mwandishi wa habari wa ITV na Radio one Stephen Wang'anyi kichukua matukio jana usiku

Basi la saibaba baada ya kunasuliwa leo asubuhi


Watu 24 wamejeruhiwa kufuatia ajali iliyotokea jana usiku majira ya saa tatu na nusu, ambapo Basi la Saibaba T687 BUW likitokea Dar es salaam kuelekea mwanza liligonga Treni ya abiria iliyokuwa inatokea Mwanza kwenda Dar es salaam katika eneola  Kalogo barabara ya kwenda Mwanza mjini shinyanga.


 Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa shinyanga Dk Fredrick Mlekwa ameiambia malunde1.blogspot.com kuwa hadi sasa kati ya majeruhi 24 waliofikishwa katika hospitali hiyo ya mkoa majeruhi waliobaki ni 6 na wengine wameruhusiwa jana na leo asubuhi.


Kamanda wa jeshi la  polisi mkoa wa shinya ACP ambaye alikuwepo katika eneo la tukio akiwa na maafisa wengine kibao was polisi amesema chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana na kwamba atatoa taarifa kamili hapo baadae kwani uchunguzi bado unaendelea.


Walioshuhudia tukio hilo wamesema ghafla walisikia sauti ya mpasuko wa taili za gari baadae kuona basi limenasa kwenye treni huku baadae maafisa wa polisi walifika na majeruhi wakikimbizwa katika hospitali ya mkoa wa shinyanga.


Dreva msaidizi wa basi hilo bwana Hussein Mohamed amesema walipofika eneo la kalogo ghafla walishtukia gari lao limeburuzwa kwa umbali wa takribani mita 30 kutoka barabarani na kuongeza kuwa treni hiyo haikupiga honi na haikuwa imewasha taa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post