Jeshi la
polisi mkoani shinyanga linamshikilia kijana mmoja aitwaye Mlaba Hamis (19) kwa
tuhuma ya kummua kwa kumpiga nondo kichwani bibi yake Mindi Doto (70) mkazi wa kijiji na
kata ya Ukenyenge tarafa ya Negezi wilayani Kishapu kutokana na kile kinachodaiwa
kuwa imani za kishirikina baada ya kijana huyo kukataa kufundishwa uchawi.
Kaimu
kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga SSP Onesmo Lyanga amesema tukio
hilo limetokea leo alfajili majira ya kumi na moja ambapo bibi hyo alikutwa
chumbani wake akiwa amefariki dunia baada ya kupigwa na mjukuu wake.
Amesema
chanzo cha tukio hilo ni imani za
kishirikina baada ya mtuhumiwa kuugua kwa muda mrefu kisha kwenda kwa mganga na
kuambiwa kuwa bibi huyo alitaka kumuua kwa kukataa kufundishwa uchawi.
Hata hivyo
Kamanda Lyanga amewaasa wananchi kuacha kabisa tabia ya kujihusisha na imani za
kishirikina.