Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde zinaeleza
kuwa huko mkoani Geita, kuna vita kati ya Waislamu na Wakristo, kufuatia
hatua ya Wakristo kuchinja mifugo kwa nia ya kuuziana wenyewe kwa
wenyewe kwenye bucha walilotenga.
Jambo hilo linaelezwa kuzua tafrani kwa jamii ya Waislamu, kwani
waliamua kuvamia eneo hilo na kuharibu bucha, pikipiki eneo hilo, na
kusababisha watu kuingilia, na vita kuibuka, silaha za jadi zikitumika.
KWANINI ?
Wakristo Mkoani Geita eneo la Katoro na Buselesele, waliamua kuachana na
kununua nyama katika bucha za kawaida kwa madaikwamba hiyo ni ibada kwa
waislamu, na hivyo wao hawako tayari kushiriki ibada hiyo, na badala
yake watafanya ya kwao. Ndipo walipokwenda Kituo cha Polisi na kuomba
kibali cha kuchinja, ambacho walipewa ilmradi wasiuze nyama hiyo.
hatimaye Wakrsito hao wakachinja na kuamua kupeleka kwenye bucha lao
ambalo wamelitenga kwa ajili ya waumini wao kununua. Waislamu kuona
hivyo, ndipo wakaenda kuripoti kituoi cha Polisi, na wakati Polisi
(wachache) wanaongea na viongozi wa Kikristo eneo hilo ili kutatua na
kurejesha amani, ndipo kundi la Waislamu likaja na kuanza kushambulia
kilichokkuwa eneo hilo, wakivunja bucha, na pikipiki ya mkristo
mmojawapo iliyokuwa eneo hilo.
Hatua hiyo imeelezwa kuibua hasia na kupelekea baadhi ya wat waliokuwa
eneo hilo kuanza kujibu mashambulizi hayo, na mpaka hivi sasa
inaripotiwa kuwa nguvu zaidi ya Jehi la Polisi haijafika eneo hilo, huku
waumini wawili wa dini ya Kiislamu wakiwa katika hali mbaya kutokana na
kipigo.
Silaha ni za jadi, na eneo hilo haliko salama kwa hivi sasa, kwani hata
amduka mengine yamefungwa kuhofia usalama wa mali na maisha.
Katibu wa umoja wa makanisa ya Katoro na
Buselesele, Mchungaji Silvanus Dominick, ameeleza kuwa kama hali
haitatulizwa mara moja basi eneo hilo laweza kuleta madhara zaidi.