BREAKING NEWS....MTUHUMIWA MAUAJI YA MWANGOSI MGONJWA


Huyu ndie mtuhumiwa wa mauwaji ya Daudi Mwangosi
MTUHUMIWA  wa  mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi askari  wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23)leo ameshindwa  kufika mahakamani katika kesi yake  baada ya kudaiwa kuwa ni mgonjwa .

Kesi   hiyo ambayo leo ilikuwa  ikifikishwa mahakamani  hapo kwa ajili ya  kutajwa  imeshindikana baada ya mahakama  hiyo  kuelezwa  kuwa mtuhumiwa   huyo ni mgonjwa na  imeshindikana  kufikishwa mahakamani hapo.
 
Mwendesha mashtaka  wa jamhuri Adolf Maganda aliieleza hakimu  wa mahakamani ya hakimu mkazi  wilaya ya Iringa Dyness Lyimo kuwa mtuhumiwa alipaswa  kufikishwa mahakamani hapo  leo  ila imeshindikana  kutoka na taarifa  kuwa ni mgonjwa  hivyo  kuomba  kupangwa  tarehe nyingine ya kutajwa  kesi hiyo ambayo  bado  upelelezi wake  kukamilika .

Hata  hivyo mahakamani  hiyo  imeahirisha  kesi hiyo  hadi Januari 31  itakapotajwa  tena .

Mtuhumiwa  huyo anatuhumiwa  kumuua kwa makusudi kwa   bomu aliyekuwa  mwandishi  wa habari wa Chanel Tena  mkoa  wa Iringa  marehemu Mwangosi  septemba 2 Septemba mwaka jana  katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa  wakati  wa vurugu kati ya  polisi na wafuasi wa  Chadema .kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai. Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002,

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post