RIPOTI MAALUM: FREEMASON NI NINI, JINSI YA KUJIUNGA, WANACHOFANYA, IBADA ZAO NA MENGINE FUATILIA HAPA

Sir Andy Chande akifanya interview na Gerald Hando wa Clouds Fm.

 

Kuna idadi kubwa ya watu waliohitaji kufahamu Freemason ni nini baada ya taarifa kuenea kwamba Freemason ni dini ya kishetani na watu wengi maarufu wamo humo wakiwemo viongozi wa nchi na mastaa wengine kama Jay Z, Rihanna, Beyonce, Kanye West, Celine Dion na hata hapa Tanzania june 2012 magazeti ya udaku yaliwataja wasanii kama Diamond Platnums na Jackline Wolper kwamba wamo humo lakini wasanii wenyewe walikanusha.

Clouds TV/Radio kupitia kwa mtangazaji Gerald Hando ilipata nafasi ya kufanya mahojiano na Sir Andy Chande ambae aliwahi kuwa kiongozi mkuu wa Freemason Afrika Mashariki kwenye nchi za Tanzania, Uganda, Kenya na Seychelles.

Yafuatayo hapo chini ni maelezo aliyoyatoa.

ALIKOANZIA SIR CHANDE:
Sir Chande: Alifika Tanzania mwaka 1950, alihamia Dar es salaam 1953 na kukutana na watu wengi wa bandarini, shirika la reli na mashirika mbalimbali aliyofanyia kazi na alikutana na watu wengi ambao walikua wanahudhuria vikao vya freemasons, akaanza kuuliziaulizia na akajifunza mambo kadhaa kuhusu hao watu.

Kwa wakati huo, hao watu hawakua huru kuzungumzia Freemasons kama anavyofanya chande sasa hivi, haswa kabla ya vita ya pili ya dunia.

Sir Chande anasema wakati huo Freemasons ilikua imegawanywa kwenye makundi tofauti, katika mahospitali, shule, na mashirika mbalimbali na kulikua na kundi maalum la freemasons kwa ajili ya matajiri na wafanyakazi wakubwa wa serikali, ukiangalia vizuri wengi wao walikua wazungu na baadhi ya wahindi.

Kundi la kwanza lilikua linaongozwa na watu wa Scotland, makundi mawili yaliyofata yalikua yanaongozwa na waingereza na kundi la nne lilikua linaongozwa na wahindi ambalo kundi la nne ndilo Chande alilojiunga nalo nalo, ilimchukua miaka miwili kukubaliwa kujiunga na freemason, aliapishwa rasmi rasmi mwaka 1954 akiwa na umri wa miaka 28, kumbuka kwamba masharti ya kujiunga na freemasons ni lazima uwe na umri kuanzia miaka 21.

Baada ya hapo ndipo alipoanza kupenda Freemasons ambapo pia alipanda cheo na kupewa nafasi ya kuongoza kundi au tawi la freemasons katika nchi nne ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda na sychels na akajiunga na miradi tofauti ya freemasons nchini uingereza yakiwemo mahoteli ya kifahari pamoja na kupewa jukumu la kujenga hoteli mpya ya freemasons nchini Ghana kwenye mji wa Khumasi ambayo ni ya kifahari sana.

Hoteli nyingine ya kifahari alisimamia ujenzi wake iko Zambia.
Sir Andy Chande kwa sasa ni mstaafu wa freemasons, 2005 alistaafu kuwa kiongozi wa Freemasons Afrika Mashariki baada ya kuifanyia kazi kwa miaka 19, kwa sasa haudhurii mikutano ya hizi nchi za Afrika Mashariki lakini anahudhuria mikutano ya Uingireza kwa sababu bado anafanya kazi na baadhi ya mashirika Uingereza.

Kanye west, Jay Z na Rihanna.

FREEMASONS NI NINI?
Ni taasisi ambayo ilianzishwa miaka 350 iliyopita katika njia ambayo haikua rasmi ikaja kuhalalishwa miaka 300 iliyopita, hatujui vizuri ilianzishwa vipi ila inaaminika walikua wajenzi wanaojenga mashule, makanisa, wakati ule kulikua hakuna miji mikubwa kama sasa wala mahoteli, na wao walikua wakiishi pamoja na familia zao na wakihama wanahama pamoja, wakaanzisha miradi ya kujenga hoteli ndogo ndogo ili kusaidiana kama wajenzi na kujikwamua kiuchumi, wakawa wanafundishana.. yani kama una ujuzi unamsaidia na mwenzako kujua
.

AnasemaFreemasons sio dini na tukikuta wewe ni mkristo tunakushinikiza ukristo wako, kama wewe ni mhindu unabaki kuwa mhindu, lakini freemasons orijino ilianzishwa na wakristo nchini Uingereza na baadae ikahamia Ulaya, Marekani, Australia na India Freemasons ikaja kuwa kubwa sana”

NCHI ZA AFRIKA AMBAZO FREEMASON NI KUBWA:
Kwa nchi za Afrika Freemasons imekuja kuwa kubwa kwenye nchi kama za Nigeria na Ghana pia Sierra Leone, kwanza aliyewahi kuwa rais wa nchi hiyo Daudi Jawala alikua mmoja wetu.

Freemasons ilianza mwaka 1646 alafu ikaja kuwa rasmi mwaka 1717 lakini kabla ya hapo katikati ilikua inafanywa kimya kimya.

KAZI ZINAZOFANYWA NA FREEMASON
Kazi zinazofanywa sasa hivi na Freemasons ni kufundisha wanachama wake kuhusu majukumu yao kwa mwenyemwezi Mungu, kwa nchi yako, familia, na nchi unayofanyia kazi hata kama ni ugenini, na kutoa misaada.

Rihanna.

WANACHAMA WA FREEMASONS DUNIANI:
Duniani kote sasa hivi kuna wanachama milioni tatu laki tano wa freemasons na wanachangia dola za kimarekani zaidi ya milioni 400 kwa ajili ya misaada kila mwaka, yani kwa siku ni zaidi ya dola milioni moja kusaidia afya, elimu vilevile wajane wa wanachama wa freemasons wanasaidiwa ambapo pia ukiumwa na ukiwa na shida yeyote kuna msaada wa bure unapatiwa nakumbuka hata dr Charles Matwali alipoumwa sana, tulimpeleka uingereza kwa matibabu.

JINSI YA KUJIUNGA NA FREEMASONS:
Ili kujiunga ni lazima uwe na umri wa miaka 21, ni hiari kujiunga na pia uwe unamwamini Mungu haijalishi ni Mungu gani, watu ambao hawamuamini Mungu hawaruhusiwi kuwa Freemasons, na lazima uwe mtu mkweli
.

Ni lazima familia yako ikubali pia wewe kujiunga na freemasons kwa sababu freemasons hawatokubali kujiunga kwako kukufanye uwe masikini kutokana na kutoa misaada.

Unapotaka kujiunga ni lazima upeleke maombi yako kwa mtu unaemfahamu ambae yuko Freemasons, au kama hujui mtu unaandika barua baada ya hapo utapewa nakala za kusoma na kuelewa na kamati ya kukuruhusu kuingia kwenye freemasons itakupeleleza wewe na familia yako, na pia watakutembelea nyumbani kuongeana mkeo au mumeo au familia.

Inaweza kuchukua mwaka mmoja na nusu au mwaka kuruhusiwa kujiunga na freemasons baada ya kupeleka maombi, ambapo hapo ni kukubaliwa tu, baada ya hapo ili uwe freemason kamili kuna vyeo vitatu ambavyo tunaviita degrees ambavyo ni lazima uvikamilishe jambo ambalo linaweza kuchukua zaidi ya miaka miwili.

.

BAADA YA KUJIUNGA:
Pia unatakiwa kujifunza vitu vingi na kuvihifadhi kichwani kama vile maneno ya kusema wakati unafanya ibada za freemasons kwa sababu tukiwa pamoja tunavyozungumzia sifa za kuwa binadamu kamili unaweza ukafananisha na ibada ya kanisani.

KUHUSU FREEMASON YA UINGEREZA:

Acha nizungumzie Freemason ya Uingereza ambayo mimi ni mmoja wao, Makao makuu yako London kwenye barabara inaitwa great queen street, Mkuu wa Freemasons Uingereza ni binamu yake malkia Elizabeth ambae tunamuita Grandmaster.

Kazi zote zinazofanyika na Freemasons zinaendeshwa kutoka kule, kwa mfano mv bukoba ilivyozama nilipiga simu kule kuomba msaada wakatuma pound elfu 10 ingawa na sisi hapa tuna kitengo chetu cha misaada ambayo kilichangia, maamuzi ya misaada mikubwa yanatoka Uingereza.

Kuna mahoteli ya freemasons Uingereza, Scotland na Ireland na katika nchi zilizokua za kisovieti zamani, tuna mahoteli duniani nzima ambapo kama upo kwenye freemasons ya Dar es salaam unaweza kuhudhuria vikao kwenye yeyote kati ya hizo hoteli duniani tunazomiliki ambazo zinatumika pia kama kumbi za mikutano yetu ili mradi wawe na uthibitisho kwamba wewe ni mmoja wetu.

Watu wengi huwa wanasema ni taasisi inayofanya mambo yake kwa siri lakini ukweli ni kwamba siri pekee iliyopo ni jinsi nitakavyokutambua kama wewe ni mmoja wetu, vingine vyote viko wazi na vinapatikana hata kwenye internet na unaweza kwenda kwenye maduka ya vitabu kote afrika mashariki hata uingereza ukapata nakala zote za freemasons ikiwemo hata maneno tunayosema tukifanya ibada zetu.

Kwa afrika Mashariki makao makuu ya freemasons yako Nairobi Kenya kwa sababu aliechukua nafasi yangu yuko Nairobi na pia makamu wake yuko Nairobi, Kuna majumba 50 ya freemasons Afrika Mashariki
Ingawa makao makuu yako Nairobi, jumba la Dar es salaam linajitegemea lenyewe na tunafanya miradi yetu na kusajili watu wetu hapahapa, hatuingiliwi na ofisi ya Nairobi, maamuzi yetu yanafanyika hapa hapa.

Hapa ni Freemasons Hall Dar es salaam ambapo Sir Chande anasema kuna masonic lodge nne Dar es salaam. (Picha imepigwa na blog ya samsasali)

FREEMASONS WANAPOKUTANA:
Huwa tunakutana saa 12 jioni na kutoa ripoti ya tulivyovifanya tangu mkutano wa mwisho, kuhusu misaada tuliyotoa, wanachama wanaoumwa, na nani wa kwenda kumtembelea au kama kuna mwananchama mpya wa kumuapisha, kama hayupo tunajadiliana kuhusu mambo tofauti yanayotuhusu isipokua siasa na dini, tunakula pamoja na kila mtu anaondoka.

MNAKUTANA MARA NGAPI?

Inategemea kama tawi la Uingereza tulikua tunakutana mara mbili kwa mwaka, la huku ambalo ndiko nilikoapishwa tulikua tunakutana mara 11 kwa mwaka lakini siku hizi ni mara kumi, wengine wanakutana mara 5, inategemea na kazi za kufanya, mfano labda wanachama wa kuapisha ni wengi.
Ibada inafanyikaje?

.

Ibada inaanza wakati vikao vinaanza, inahusisha mara nyingi kitu ambacho kinafanana na ibada kanisani, mara nyingi inahusika kumuweka mwananchama mpya kwenye mstari na mtazamo mmoja na aliowakuta na kwenye ibada huwezi kuvaa unavyotaka, lazima uvar suti na tai isipokua nchi kama India ambao hawavai tai.

Ukiwa mwanachama unapewa maswali ambayo ukiyajibu vizuri kwa muda wako unaweza kupandishwa cheo na inachukua muda kufikia degree ya tatu, tukiwa kwenye vikao mwenyekiti anaitwa Master na anao wasaidizi wawili, kwenye ibada mwenyekiti anakaa mashariki, msaidizi mmoja ana kaa mbele yake akimtizama na wa pili anakua anasaidia kwa shughuli nzima inayoendelea.

Kuna mwingine ambae ndio muongozaji wa sala na wakati tukisali, Mungu tunamuita Fundi mkuu aliyeumba sayari zote hiyo inahakikisha kwamba uwe Musilamu au mkristo tunakwenda sambamba.

ISHARA ZINAZOTUMIKA FREEMASONS

.

.

Kuna alama ya Compass inayotumika kuonyesha mwelekeo kwa mishale yake, kuna ruler na pembe nne ambavyo ni vitu vinavyotumika kwenye ujenzi ila vinaweza kutumika kufundisha kuhusu maisha, na ndio vinatumika hivyo wala sio kuhusu kitu kingine.

Tukifanya ibada zetu au kumkubali mtu kuingia freemasons lazima avae pajama au mavazi yanayotumika kulalia usiku, na haruhusiwi kuwa na pesa mfukoni, kuvaa saa au cheni ishara ya kuwa yeye ni masikini kama alivyozaliwa.

Uchawi, kuabudu shetani na mambo kama hayo watu wanayosema kwamba freemasons ndio inajihusisha na hivyo vitu ikiwemo kutoa uhai ndugu, ni waongo, hawana ujuzi wa kutosha, nakumbuka pia rais Moi aliunda kamati maalum kuchunguza uchawi na waabudu shetani na tuliitwa nikaenda kuwaeleza kwa muda wa karibu saa na nusu kuhusu freemasons, ingawa hawakuja kutupa ripoti kamili waliyopeleka kwa rais moi, walituambia kwamba wamekubali maelezo yetu na ingekua bora kama tungekua tunaeleza zaidi watu wajue na tusiwe wasiri.

FAIDA ZA KUWA FREEMASONS:
Hakuna faida za kupata pesa kama wengi wanavyoambiwa kwamba ukiwa freemasons unapewa mihela, faida za kuwa freemasons ni pamoja na kuongeza idadi ya marafiki na kuongeza knowledge (ufahamu)

Faida nyingine labda ni kama ukitoa tenda kama unaanzisha kiwanda na umetoa tenda ya kazi, ukiona mmoja wa freemasons yuko kwenye list ya walioomba tenda utampa kipaumbele kwa sababu unamfahamu na ni kama ndugu.

Hakuna utoaji wa kafara kama inavyosemekana na pia hakuna uhusiano kati ya freemasons na agano la kale.

MAMA MZAZI WA KANUMBA KUHUSU KANUMBA KUWA FREEMASON:

Mama mzazi wa Marehemu mwigizaji Steven Kanumba alisema siku kadhaa baada ya Kanumba kufariki kuna kijana alikuja nyumbani na kumwambia mama kwamba yeye (kijana) ndio alimsaidia Kanumba kujiunga na Freemasons miaka kadhaa iliyopita hivyo alikwenda nyumbaniili wazungumze na mama, mama Kanumba alimfukuza hapohapo na kumwambia mwanae hajawahi kuwa freemason na akamwambia akirudi tena atamwitia polisi.

.

MISTARI YA JAY Z KWENYE WIMBO WA FREEMASON WA RICK ROSS.

Watu wananisingizia mambo ya kishetani, uvumi unaenea sehemu zote,  nipishe huyu ni Mungu anafanya mambo yake, najua mnaniogopa Sijui wa kumwamini sala ya maria inafanya kazi.

Mnanisingizia vitu vingi vya kishetani lakini bado mnapandisha sauti kubwa mkisikiliza muziki wangu, hizo stori zote hazina msingi, mniache Mungu anafanya kazi yake.

Mungu ndio injinia hapa, asiefanya fanya dhambi atupe jiwe la kwanza angalieni sura zenu kwenye vioo mnavyoonekana, Sio kwamba mimi ni Freemason, nilipitia tu mambo mengi sana na Mungu anisamehe manake nisingefika nilipo bila kufanya dhambi, nimeosha sura yangu kwa maji matakatifu hii rozari yenye shanga, tena shanga za diamond ni uthibitisho kwamba Mungu alinisamehe.

Mi ni mkali, acha kutazama kwenye sahani yangu… sema tu unatamani nilichonacho.

RIPOTI YA CNN AUGUST 2010 KUHUSU FREEMASON:

Baadhi ya maseneta wa majimbo kadhaa ya Marekani walikiri kuwa ni wanachama wa Freemason ambapo ilifahamika kwamba Marais 12 waliowahi kuiongoza Marekani walikua wanachama wa Freemason ambapo pia watu 9 kati ya waliosaini hati ya uhuru wa Marekani walikua freemason akiwemo George Washington. 

SOURCE: millardayoblog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments