MAELFU YA WATU WAJITOKEZA KUMZIKA ASKOFU BALINA-SHINYANGA,SHUHUDIA TUKIO ZIMA


ASKOFU BALINA ENZI ZA UHAI WAKE
                                                          

VIONGOZI WA DINI WAKIFUATILIA IBADA YA MAZISHI ILIYOFANYIKA LEO KATIKA KANISA LA MAMA MWENYE HURUMA NGOKOLO MJINI SHINYANGAKATIKATI NI MAMA WA MAREHEMU ASKOFU BALINA BIBI TERESIA NIGO MWENYE UMRI WA MIAKA ZAIDI YA 90 LEO KATIKA KANISA LA MAMA MWENYE HURUMA LA NGOKOLO MJINI SHINYANGA


WA PILI KUTOKA KUSHOTO NI MBUNGE WA JIMBO LA SHINYANGA MJINI,AMBAYE PIA NI NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI STEVEN MASELE


 

IBADA INAENDELEA

IBADA INAENDELEA KANISA LIMEJAA WENGINE WAKO NJEIBADA INAENDELEA KANISA LIMEJAA WENGINE WAKO NJERAIS KIKWETE AKITOA SALAMU ZA RAMBI RAMBI LEO
KABURI LAKE KABLA YA MAZISHIKATIKATI NI JENEZA LILILOBEBA MWILI WA MAREHEMU ASKOFU BALINA

MAZISHI YANAENDELEA
MAZISHI YANAENDELEA

SHUGHULI YA KUWEKA MASHADA INAENDELEA

WALIOHUDHURIA MAZISHI WAANZA KUTAWANYIKA BAADA YA MAZISHI                                                      PICHA ZOTE NA MALUNDE KADAMA


                                         MSIMAMIZI WA JIMBO ATEULIWA

Baba Mtakatifu Papa Benedicto wa 16 amemteua Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza Mhashamu Yuda Thadeus Ruwaichi kuwa msimamizi wa kitume wa Jimbo la Shinyanga ,mpaka atakapoteuliwa Askofu mwingine,kufuatia kifo cha aliyekuwa Askofu wa Shinyanga Aloysius Balina aliyefariki dunia Novemba 6 2012.

Kwa mujibu wa barua ya Baba Mtakatifu iliyosomwa leo na Balozi wa Vatican nchini Tanzania,Askofu Mkuu Fransisco Padila na kufuatia uteuzi huo, Askofu Mkuu Ruwaichi amemteua Padre  Sospita Shole ,ambaye ni paroko wa parokia ya Shinyanga Mjini kuwa mratibu wa shughuli zote za kanisa jimboni.

Mazishi ya aliyekuwa Askofu wa jimbo Katoliki la Shinyanga marehemu Aloysius Balina yamefanyika leo katika Kanisa Kuu la Mama Mwenye Huruma la Ngokolo Mjini Shinyanga na yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini,vyama vya siasa na serikali akiwemo rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post