MWENYEKITI WA CHADEMA ACHOMWA MKUKI -SHINYANGA

Mwenyekiti wa CHADEMA tawi la Mwawaza katika Manispaaa ya Shinyanga bwana Bundala Katunge amejeruhiwa vibaya baada ya kuchomwa mkuki tumboni na watu wasiojulikna usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake.

Walioshuhudia tukio hilo wamesema mwenyekiti huyo wa chadema akiwa amelala nyumbani kwake majira ya saa tano  alisikia kelele za watu nje ya nyumba yake  na baada ya kutoka nje alikuta kundi la watu wakishusha bendera ya chama hicho iliyotundikwa hapo na waliomuona wakakimbia na mmoja wao kumchoma na mkuki ubavuni.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa Dr Fredrick Mlekwa amesema wamempokea majeruhi huyo na kumfanyia oparesheni na hali yake amesema inaendelea vizuri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments