Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limesema chanzo cha mwenyekiti wa Chadema Tawi la Lubaga katika Manispaa ya Shinyanga,Bundala Katunge kuchomwa Mkuki tumboni ni ushabiki wa kisiasa kati yake na kundi la watu ambao miongoni mwao aliwatambua na wote wamekamatwa kwa mahojiano zaidi.
Kamanda wa polisi mkoa wa shinyanga ACP Evarist Mangalla amewaja wanaoshikiliwa kuwa ni Bundala Masanja,Benjamini Kanena,Magembe Makonda na Martine Mashimbi wote wakazi wa Mwawaza.