MOHAMED IDD CONTROL AFARIKI DUNIA
TANZIA, Mpiga gitaa mahiri MOHAMED IDD aka "CONTROL" amefariki
dunia leo alfajiri. Wakati wa uhai wake marehemu amewahi kupigia bendi kadhaa zikiwemo
Double O ya King Kiki, National
Panasonic, Mlimani Park, OTTU na alienda kufanya kazi Uarabuni na Zanzibar Sound ya Asia Darwesh.
Baada ya
kukaa Uarabuni kwa muda aliamua kurejea bendi yake ya zamani ya Sikinde.
Miongoni mwa vibao vilimpatia umaarufu ni pamoja na wimbo Gloria wa OTTU ambao
alipiga solo. R.I.P IDD CONTROL