MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU AJINYONGA KWA KUTUMIA KAMBA YA VIATU, SHUHUDIA
Mwili wa Mwanafunzi wa darasa la tatu, Shule ya Msingi Iwambi, Jijini Mbeya Kervin Patrick (8) jinsi ya kiume ukiwa umefunikwa baada ya kufariki dunia kutokana na kujinyonga kwa kutumia kamba ya viatu katika bomba ya maji nje ya nyumba yao.
Baadhi ya majirani waliojitokeza kushuhudia mwili Mwili wa Mwanafunzi wa darasa la tatu, Shule ya Msingi Iwambi, Jijini Mbeya Kervin Patrick (8)
Mama
mzazi wa marehemu Kervin Patrick (8)Bi Subira Patrick(38) akiwa katika
hali ya majonzi kufuatika kifo cha mwanae aliyejinyonga.
Picha na Ezekiel Kamanga
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Picha na Ezekiel Kamanga
Na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Mwanafunzi
wa Shule ya Msingi Iwambi, darasa la tatu Kervin Patrick (8) jinsi ya
kiume amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya viatu
katika bomba ya maji nje ya nyumba yao.
Tukio
hilo limetokea Oktoba 27 mwaka huu majira ya saa 5 kamili usiku wakati
wazazi wote wa mtoto huyo Bwna Patrick Mwakapalila(52) na Bi Subira
Patrick(30) wakiwa hawapo nyumbani na kwamba baba mzazi akiwa na mwanae
wa kiume aitwaye Joshua Patrick(10) waliondoka majira ya saa 3:30
kuelekea mjini.
Aidha
Baba wa mtoto huyo alipigiwa simu na mtu mmoja kwamba arejee nyumbani
na yeye pasipo kuchelewa alirejea na kumkuta mwanae amejinyonga katika
bomba la maji kwa kutumia kamba ya viatu na chini kukiwa na ndoo, ambapo
kifo hicho kimezua maswali mengi kwani kimo cha mtoto ni zaidi ya futi
mbili na nusu na urefu wa kamba hali inayotia shaka kuwa mtoto huyo
alichukua uamuzi huo yeye mwenyewe.
Mwenyekiti
wa Mtaa wa Ivwanga Bwna Chonde Kalisto amethibitisha tukio hilo la
kusikitisha na kwamba yeye alipokea taarifa kutoka kwa Balozi wake Bi
Esther Mahenge ambapo walitoa taarifa polisi ambapo walifika eneo la
tukio kisha kuuchukua mwili wa marehemu kwa uchunguzi zaidi na hakuna
mtu yeyote anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo.