WEZI WA NYWELE WAZUA BALAA...WANAWAKE WAKATWA NYWELE WAKIWA WAMEPOTEZA FAHAMU

Sunita Devi

Zaidi ya wanawake 50 katika majimbo yaliyo Kaskazini mwa India ya Haryana na Rajasthan wamesema kuwa wamekatwa nywele zao wakati wakiwa hawana fahamu.

Polisi wanajikakamua kutatua visa hivyo ambayo vinawaacha wanawake na mshutuko mkubwa.

"Kulikuwa na mwanga mkali uliosababisha nipoteze fahamu. Saa moja baadaye niligundua kuwa nywele pia ikuwa imekatwa," alisema Sunita Devi, mwanamke mwenye umri wa miak 53 kutoka Haryana.

"Nimeshindwa kulala wala kufanya chochote. Nilisoma kuhusu visa hivi vikifanyika huko Rajasthan, lakini sikufikiria kingetendeka kwangu," aliongeza Sunita.Munesh Devi anasema kuna hofu katika jamii

Mbali kidogo mwanamke mwingine Asha Devi naee alipoteza nywele yake katika shambulizi kama hilo siku iliyofuata.

Lakini wakati huo mshambuliaji aliripotiwa kuwa mwanamke.

Baba mkwe wake Asha Devi, Suraj Pal anasema kuwa kufuatia kisa hicho, alimshauri pamoja na wanawake wengine wa familia kuhamia nyumba ya jamaa wao katika jimbo la Uttar Pradesh.Mashambulizi hayo pia yamefanyika mjini Delhi.

Bwana Pal anasema alikuwa nyumbani wakati Asha Devi alitoka nje kufanya kazi zake.

"Nilienda nje kujua ni kwa nini hakurudi baada ya zaidi ya dakika 30. Tulipmkuta amepoteza fahamu katika chumba cha kuoga. Nywele zake izlikuwa zimekatwa na kutupwa sakafuni."alisema.

Ripoti za kunyolewa wanawake kwanza ziliibuka mapema Julai kutoka jimbo la Rajasthan, lakini visa sawa na hivyo kwa sasa vinaripotiwa kutoka Haryan na hata mji mkuu Delhi.Sundar Devi, 60, amekuwa kitandani tangu ashambuliwe Jumamosi

Sunita Devi anaishi katika jamii ya wafanya biashara na wakulima.

Baadhi wa majirani zake wanachukua zamu kukaa naye hadi apate kuondokewa na mshutuko.


Anasema mshambuliaji wake alikuwa ni mwanamume mzee ambaye alikuwa amevaa nguo nyeupe.Wanawake kutokaa sehemu za Delhi wamekuwa wakitumia picha na miungu ili kulinda nywele zao.
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post