RAIS MAGUFULI : WAKATI WANGU HAKUNA KUPATA PESA KWA NJIA RAHISI LAZIMA UFANYE KAZI KWELI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka na kusema katika wakati wake hakuna kupata pesa kwa njia rahisi kwani lazima ufanye kazi kweli ili kupata pesa halali.


Rais Magufuli amesema hayo leo Handeni wakati anaelekea mkoani Tanga kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Chongoleani Tanga Utaofanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 05 Agosti mwaka huu.


"Kuna watu walikuwa wamezoea vya bure wanapiga 'disco' tu wanapewa hela nyingi hazipo pesa za namna hiyo, hivi sasa watu wanataka ufanye kazi uzalishe mali ili upate fedha za kweli na asiyefanya kazi asile na usipokula maana yake ufe" alisisitiza Rais Magufuli


Mbali na hilo Rais Magufuli amesema uchumi wa Tanzania unakuwa kwa kasi kubwa na kudai kwa Afrika katika nchi tano ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi kubwa Tanzania pia ipo imeshika nafasi ya pili nyuma ya Ethiopia.


"Ikiwa uchumi wetu unakuwa kwa asilimia 7.2% wapo watu watakuja na kulalamika hela zimepotea, hao walikuwa wamezoea vya bure, na hao ndiyo mnawaona wanapiga kelele" alisema Magufuli.


Kwa mujibu wa benki ya Dunia katika nchi ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi kubwa Tanzania imekuwa nafasi ya tano chini ya India, Nepal, Uzbekistan na Ethiopia ambayo ndiyo imekamata nafasi ya tano. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post