Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAFANYABIASHARA KARIAKOO, MACHINGA COMPLEX WASISITIZWA KUWEKA AKIBA.


Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo amewashauri wafanyabiashra kutumia vema mapato wanayo yayapata na kuhakikisha kuwa wanaweka akiba katika biashara zao kitu kitakachowawezesha kukuza kipato chao, kufanya maendeleo na biashara zao kuwa endelevu zao zaidi.

Mhe. Mpogolo ameyasema hayo leo wakati akihitimisha bonanza la michezo lililoandaliwa na Shirika la Masoko ya Kariakoo huku likihusisha wafanyabiashara wa Soko la Machinga lilipo Jijini Dar es Salaam huku akiongeza kuwa japo biashara hizo ni zao wanao wajibu wa kupata faida na kujilipa mishahara.

Ameupongeza uongozi wa shirika hilo kwa kuandaa bonanza hilo na kuongeza kuwa wafanyabiashara hao wanapaswa kutumia fursa zitokanazo na bonanza hilo kukuza ushirikiano, urafiki na fursa za biashara baina yao kwa kuwa serikali imeshaweka mazingira wezeshi na kwa wafanyabiashara.

Aidha, ameongeza kuwa Serikali itaendelea kujenga masoko ili kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wanafanya biashara katika mazingira rafiki, yenye utu na yanayojali staha kwa wafanyabiashara na kuongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia ameagiza kujengwa na kukamilika kwa Soko la wamachinga ndani ya miezi sita na kubainisha kuwa soko hilo litajengwa eneo la Kigogo Sambusa.

Kwa upande wke Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo, CPA. Ashraph Abdulkarim amesema bonanza hilo limelenga kukuza urafiki, umoja na mshikamano baina ya watumishi, wafanyabiashara wa Kariakoo, na wafanyabiashara wa Soko la Machinga Complex.

Ameongeza pia michezo ni sehemu ya kukuza upendo, mshikamano na Amani na pia kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza kwa kuepuka tabia bwete kwa kufanya mazoezi na kuahidi mabonanza kama hayo yatakuwa endelevu.

Katika bonanza hilo timu ya mpira wa miguu na mpira pete walishinda na kupata medali, kombe na fedha huku Shirika la Masoko ya Kariakoo likipata medali katika michezo ya mpira wa miguu na pete na pia kupata kombe kwenye mchezo wa kuvuta Kamba.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com