📌Tanzania yawakilishwa vyema jukwaa la biashara Afrika kwa kunadi fursa za uwekezaji;
📌Nchi za Afrika zaaswa kushirikiana kwa pamoja kuongeza mnyororo wa thamani wa bidhaa zao;
📌Naibu Waziri Mkuu wa Ethiopia azitaka nchi za Afrika kushirikiana na kutumia fursa ya soko la Afrika kuuza bidhaa zao na kuongeza thamani kwenye bidhaa zao;
Addis Ababa, Ethiopia.
Naibu Waziri Mkuu wa jamhuri ya watu wa Ethiopia Mhe. Temesgen Tiruneh leo amefungua rasmi mkutano wa jukwaa la maendeleo ya biashara jijini Addis Ababa nchini Ethiopia wenye lengo la kujadili fursa za biashara kwa nchi za Afrika na namna nchi hizo zinavyoweza kutumia fursa ya soko la Afrika kuuza bidhaa zake, na kujadili changamoto mbalimbali zinazosababisha nchi za Afrika kushindwa kutumia fursa za masoko ya Afrika na namna ya kuzitatua kwa pamoja.
Amesema nchi nyingi za Afrika zina bidhaa nyingi na zinazalisha bidhaa nyingi na za kutosha kwa ajili ya mauzo, ila changamoto kubwa nikuuza bidhaa ambazo hazijachakatwa na hivyo kuzikosesha mapato nchi zao na kuwataka Mawaziri wa Afrika walioko kwenye jukwaa hilo kuhakikisha wanauza mazao yenye kuongeza mnyororo wa thamani na kutumia vema soko la Afrika kuuza bidhaa zao.
Mkutano huo wa jukwaa la maendeleo ya biashara kwa nchi za Afrika ulioandaliwa na Serikali ya Ethiopia kwa kushirikiana na Trademark Afrika unashirikisha Mawaziri wa Viwanda, Biashara na utengamano wa kibiashara kutoka nchi za Afrika na wadau mbalimbali wa uwekezaji kutoka nje ya nchi, una lengo la kujadili fursa za uwekezaji kwa Afrika na kutatua changamoto za kibiashara kwa Afrika na namna ya kuzitatua.
Sambamba na jukwaa hilo, pia ilizinduliwa ripoti ya maendeleo ya biashara kwa nchi za Afrika kwa mwaka 2026.
Tanzania inashiriki kwenye mkutano huo na kushirikisha Wizara ya Viwanda na biashara ambapo Naibu Waziri wa Viwanda na biashara Mhe Dennis Londo anaongoza ujumbe unaoshiriki mkutano huo sambamba na taasisi za TANTRADE na TBS, katibu Mkuu wizara ya Fedha Dkt. Natu Mwamba, ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia, wadau wa sekta binafsi na wafanyabiashara.
















TAFUTA HABARI
Social Plugin