Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAANDALIZI YA MKUTANO WA 11 WA APS-HRMnet YAFIKIA ASILIMIA 90, WASHIRIKI 1,200 WAJIANDIKISHA



Rais wa Mtandao wa Mameneja wa Rasilimaliwatu katika Sekta ya Umma Barani Afrika (APS-HRMnet), Xavier Daudi, amesema maandalizi ya Mkutano wa 11 wa APS-HRMnet 2026 yanayotarajiwa kufanyika katika Hoteli ya Verde, Zanzibar, yamekamilika kwa asilimia 90.

Amesema mwitikio wa washiriki umekuwa mkubwa kuliko matarajio ya awali, ambapo idadi ya washiriki 800 iliyokadiriwa mwanzoni imeongezeka hadi kufikia takribani 1,200 waliojiandikisha kushiriki mkutano huo.

Daudi amesema mwitikio huo unatokana na Tanzania, hususan Zanzibar, kuwa mwenyeji wa mkutano huo, akieleza kuwa eneo hilo ni kivutio cha utalii, lina mazingira salama, watu wakarimu na linazingatia viwango vya juu vya kidiplomasia.

Aidha, amewataka washiriki kutoka ndani ya Tanzania kuanza kuwasili Zanzibar Novemba 8, 2026 kwa ajili ya kuchukua vifurushi vyao vya mkutano, huku washiriki kutoka nje ya nchi wakitarajiwa kufanya hivyo Novemba 9, 2026 katika eneo la mkutano, Hoteli ya Verde.

Ameeleza kuwa zaidi ya nchi 20 za Afrika zinatarajiwa kushiriki mkutano huo, zikiwemo nchi zitakazotuma mawaziri na makatibu wakuu wenye dhamana ya kusimamia masuala ya utumishi wa umma.








Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com