Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PSSSF YASHIRIKI BONANZA LA TANO LA AFYA LA WAAJIRI

 



Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Dkt. Eveline Munisi (kushoto) akimkabidhi Meneja wa Mfuko wa PSSSF, Kanda ya Ilala, Bi. Amina Kassim cheti cha shukrani kwaniaba ya mfuko kwa kuwa miongoni mwa Taasisi wezeshi Tamasha la Tano la Waajiri Afya Bonanza kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, Oktoba 24, 2026


Afisa Mkuu wa Huduma kwa Wateja Mfuko wa PSSSF Bi. Nelusigwe Mwalugaja (kushoto), akimuhudumia mteja Bi. Nuru A. Mwakivuma wa WCF, kujiunga na PSSSF Kiganjani katika banda la mfuko kwenye Bonanza la Tano la Afya la Waajiri, maarufu kama Waajiri Health Bonanza, lililofanyika Oktoba 24, 2026, katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, eneo la Mlimani, jijini Dar es Salaam.


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Dkt. Eveline Munisi akimvisha medali Afisa Matekelezo Mwandamizi wa Mfuko wa PSSSF Bw. Salum salum baada ya kushina mbio za kukimbia na glasi ya maji kwenye Bonanza la Tano la Afya la Waajiri, maarufu kama Waajiri Health Bonanza, lililofanyika Oktoba 24, 2026, katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, eneo la Mlimani, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Dkt. Eveline Munisi akimpongeza mfanyakazi Mwanafunzi wa Mfuko wa PSSSF Bi. Prudensiana sondoka, baada ya kumvisha Medali baada ya kushina mbio za kukimbia na glasi ya maji kwenye Bonanza la Tano la Afya la Waajiri, maarufu kama Waajiri Health Bonanza, lililofanyika Oktoba 24, 2026, katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, eneo la Mlimani, jijini Dar es Salaam.



Meneja wa Mfuko wa PSSSF, Kanda ya Ilala, Bi. Amina Kassim (katikati) na baadhi ya watumishi wa Mfuko Huo, akiwa amekamata cheti cha shukrani kwa Mfuko kuwa miongoni mwa Taasisi wezeshi Tamasha la Tano la Waajiri Afya Bonanza kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, Oktoba 24, 2026


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Dkt. Eveline Munisi, akizungumza katika Bonanza la Tano la Waajiri Afya Bonanza kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, Oktoba 24, 2026


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Dkt. Eveline Munisi (Wapili kushoto) akimsikiliza Meneja wa Mfuko wa PSSSF, Kanda ya Ilala, Bi. Amina Kassim alipotembelea Banda la Mfuko kwenye Maonesho ya Bonanza la Tano la Afya la Waajiri 'Waajiri Afya Bonanza' kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, Oktoba 24, 2026

Afisa Matekelezo Mkuu Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Bi. Zainab Ndullah (Kulia), akimuhudumia Mwanachama wa Mfuko Bw. Emmanuel Ikongwe toka Association of Tanzania Employers- ATE, kwenye Bonanza la Tano la Waajiri (5th Waajiri Health Bonanza kwenye viwanja vya Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, Sehemu ya Mlimani Oktoba 24, 2026.

Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeshiriki katika Bonanza la Tano la Afya la Waajiri, maarufu kama _Waajiri Health Bonanza,_ lililofanyika Oktoba 24, 2026, katika Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, eneo la Mlimani, jijini Dar es Salaam.

Bonanza hilo ambalo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi Ajira na Mahusiano Mhe Dkt. Evelin Munisi liliratibiwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), lengo likiwa ni kuhamasisha wafanyakazi kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi kwa ajili ya kuimarisha afya zao, kuongeza tija kazini na kukuza uhusiano mwema miongoni mwa waajiri na taasisi mbalimbali nchini kupitia michezo na burudani.

Mhe. Dkt. Munisi alizindua Bonanza hilo kwa kupiga mpira, kisha kutembelea mabanda ya Maonesho.




Akiwa katika Banda la PSSSF, Mhe. Dkt. Munisi alipokelewa na Meneja wa Mfuko wa PSSSF Kanda ya Ilala Bi. Amina Kassim.




Akizungumza mbele ya Mhe. Dkt. Munisi, Meneja huyo wa PSSSF , alisema kuwa ushiriki wa Mfuko katika bonanza hilo ni sehemu ya kuimarisha uhusiano na wadau wake, huku ukiwapa washiriki fursa ya kupata elimu kuhusu huduma za hifadhi ya jamii.




Alisema kuwa pamoja na kushiriki katika michezo mbalimbali, pia Mfuko unatoa huduma na elimu kuhusu hifadhi ya jamii.




"Tunafurahi kuungana na wadau wetu katika bonanza hili. Tunatoa elimu kuhusu huduma zetu, hususan mafao yanayotolewa na Mfuko, chini ya kaulimbiu yetu ya 'Tunalipa jana', ambayo imeufanya mfuko kwenda _Extra Mile_ katika ulipaji wa Mafao." alisema Bi. Kassim.

Aidha PSSSF imefanikiwa kutwaa medali mbili katika mbio za kukimbia na glasi ya maji kwa wanawake na wanaume, ambapo Mhe. Dkt. Munisi aliwakabidhi tuzo washindi hao.

Mwisho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com