Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

FEDHA SI KIKWAZO KUKAMILIKA KWA SGR NYAHUA–TABORA



Na Sheila Ahmadi, Tabora

SERIKALI imetoa zaidi ya Sh trilioni 3.6 kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR katika kipande cha Nyahua–Tabora huku Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa changamoto iliyopo katika utekelezaji wa mradi huo ni mipango ya mkandarasi badala ya upatikanaji wa fedha.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo Uliopo Nyahua mkoani Tabora Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amesema mkandarasi anapaswa kuboresha mipango na usimamizi wa kazi ili kuhakikisha utekelezaji wa mradi unaendana na ratiba iliyowekwa na kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Kupitia mradi huo unaendelea kutekelezwa na unatarajiwa kukamilika mwaka 2028 hivyo ni muhimu kwa mkandarasi kuhakikisha rasilimali zilizopo zinatumika ipasavyo ili kuongeza kasi ya kazi na kuepusha ucheleweshaji usio wa lazima.

Adha Profesa Mbarawa amesisitiza kuwa uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali unapaswa kuendana na mipango madhubuti ya utekelezaji, ili kuhakikisha kazi zinafanyika kwa ufanisi na kwa kuzingatia muda uliopangwa.

"Mradi huo unahusisha njia za reli za Route 3 na Route 4 huku kipande cha Nyahua kikigawanywa katika maeneo matano ya utekelezaji kwa lengo la kurahisisha usimamizi na uendelezaji wa shughuli za ujenzi " Amesema Profesa Mbarawa

Katika Hatua nyingine Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kuimarisha miundombinu ya usafirishaji nchini na kuboresha huduma za usafiri wa reli ya kisasa, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa abiria na mizigo.

Vilevile Serikali inaendelea kusimamia utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha unakamilika mwaka 2028 kama ilivyopangwa huku mkandarasi akitakiwa kuimarisha mipango na usimamizi wa kazi ili kufikia malengo yaliyowekwa.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com