Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Zanzibar
KIZIMKAZI Kumenoga! Hiyo ndio kauli mbiu iliyobeba Tamasha la Kizimkazi 20226 linatarajiwa kufanyika kuanzia Agosti 12 hadi Agosti 14 mwaka huu likiwa limesheheni fursa lukuki .
Katika tamasha hilo ambalo limejizoelea umaarufu mkubwa pia kutakuwa maonyesho, burudani na programu mbalimbali za kuvutia zinazolenga kutangaza utalii, uwekezaji na utamaduni wa Kizimkazi.
Akizungumza kuhusu maandalizi ya kuelekea tamasha hilo Wilaya ya Kusini Unguja visiwani Zanzibar leo Julai 8,2026 Mwenyekiti wa Kamati ya Tamasha la Kizimkazi Mahfodh Said Omar amesema katika tamasha hilo miradi mbalimbali ya maendeleo itazinduliwa.
Katika uzinduzi wa tamasha la Kizimkazi litafunguliwa rasmi na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk.Ali Hussein Mwinyi na kisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni katika siku ya kufunga tamasha hilo.
“Tunawaalika wawekezaji, wadau wa mandeleo, wafanyabiashara, wadau wa utalii na wananchi kwa ujumla kushiriki Kizimkazi Festival 2026, kwani mwaka huu tamasha limenoga na limebeba fursa nyingi kwa wote.
“Leo tunazindua rasmi maandalizi ya Kizimkazi Festival 2026. Tamasha hili lilianzishwa na wazee pamoja na wananchi wa Kizimkazi kwa lengo la kuhifadhi na kuenzi utamaduni, mila na desturi za eneo letu. Kadiri miaka ilivyopita, tamasha limeendelea kukua na sasa limekuwa jukwaa muhimu la kutangaza utalii,
uwekezaji na mendeleo ya jamii.
“Kizimkazi Festival ni tamasha la wananchi wa Kizimkazi. Dhamira yake ni kuitangaza Kizimkazi kama eneo lenye historia, utamaduni, vivutio vya
utalii na fursa nyingi za uwekezaji kwa manufaa ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ujumla.”
Kuhusu malengo ya Tamasha la Kizimkazi amesema ni kutangaza fursa za uwekezaji, kutangaza vivutio vya utalii pamoja na kuhifadhi na kuenzi utamaduni wa Kizimkazi.
Wakati kwa upande wa fursa za uwekezaji ni Utalii na hoteli, Uchumi wa Buluu, Uvuvi, Biashara na huduma mbalimbali, pamoja na miradi mingine ya mandeleo.
Akizungumzia miradi itakayozinduliwa wakati wa tamasha la Kizimkazi ni uzinduzi wa mradi wa maji Kizimkazi, uzinduzi wa kiwanja cha watoto Kibu Teni,ufunguzi wa nyumba za kuishi Bopar Enterprises, Jiwe la msingi Salaam Cane Restaurant-K/Dimbani.
Miradi mingine itakayozinduliwa ni mradi wa mabweni mapya -Hasnu Makame Sekondari-Kibuteni ,jiwe la msingi jengo la maendeleo Kibuteni na uzinduzi wa hoteli la kitalii ya Johari-K Mkunguni
Akielezea zaidi amesema pia kupitia tamasha hilo wanatangaza fursa za uwekezaji, vivutio vya utalii pamoja na kuhifadhi na kuenzi utamaduni wa Kizimkazi.
Ametumia nafasi hiyo kuelezea kupitia tamasha hilo manufaa yanayopatikana ni kuvutia uwekezaji, kuongeza watalii, ajira, biashara, mapato ya wananchi na Serikali, na kuchangia uchumi wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Tunawakaribisha wawekezaji, wadau wa utalii, tour operators, tour guides, travel agencies, wadhamini, vyombo vya habari, wasanii, watu mashuhuri na wadau wa maendeleo kushiriki Kizimkazi Festival ili kujionea fursa na kushiriki kuitangaza Kizimkazi duniani.”
Mwenyekiti huyo wa maandalizi tamasha la Kizimkazi amesema ujumbe mkuu katika tamasha hilo inasema Kizimkazi Festival si tamasha la burudani pekee; ni jukwaa la maendeleo linalounganisha utamaduni, utalii na uwekezaji kwa manufaa ya Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Karibuni Kizimkazi Festival mshuhudie utajiri wa utamaduni wetu, mjionee fursa za uwekezaji na vivutio vya utalii, na muwe sehemu ya safari ya kuijenga Kizimkazi kuwa kitovu cha maendeleo.”






Social Plugin