
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, akikabidhi madawati katika Shule ya Msingi Mbizi iliyopo wilayani Kakonko, mkoani Kigoma


Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, akizungumza na wanafunzi, walimu na wananchi katika Shule ya Msingi Mbizi wilayani Kakonko, mkoani Kigoma, wakati wa hafla ya kukabidhi madawati yaliyotolewa na Benki ya CRDB


Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, akizungumza na wanafunzi, walimu na wananchi katika Shule ya Msingi Mbizi wilayani Kakonko, mkoani Kigoma, wakati wa hafla ya kukabidhi madawati yaliyotolewa na Benki ya CRDB
***
CRDB YAENDELEA KAMPENI YA 'CRDB-KETI JIFUNZE', YAKABIDHI MADAWATI SHULE TATU KIGOMA NA GEITA
Benki ya CRDB imeendelea kutekeleza kampeni yake ya CRDB-Keti Jifunze kwa kukabidhi madawati katika shule tatu za msingi, zikiwemo Shule ya Msingi Mbizi wilayani Kakonko mkoani Kigoma, Shule ya Msingi Nguvu Kazi iliyopo Runzewe wilayani Bukombe mkoani Geita na Shule ya Msingi Mruba wilayani Chato mkoani Geita, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi nchini.
Madawati hayo yamekabidhiwa na Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, ambaye amesema benki hiyo inaendelea kutambua umuhimu wa elimu kama nguzo ya maendeleo ya Taifa, ndiyo maana imeendelea kuwekeza katika kuboresha miundombinu ya kujifunzia katika shule mbalimbali.
Wagana amesema Benki ya CRDB itaendelea kushirikiana na Serikali pamoja na wadau wengine wa maendeleo katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu kupitia utekelezaji wa miradi yenye manufaa kwa wanafunzi na jamii.
"CRDB tunaamini kuwa uwekezaji katika elimu ni uwekezaji katika mustakabali wa Taifa. Tunajivunia kushiriki kuboresha mazingira ya kujifunzia kwa watoto wetu ili wapate nafasi ya kutimiza ndoto zao na kuwa viongozi wa baadaye," amesema Wagana.
Ameongeza kuwa ugawaji wa madawati hayo utasaidia kupunguza uhaba wa samani katika shule husika, kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na kuboresha mazingira ya kujifunzia, hali itakayochangia kuongeza ufaulu na kuinua kiwango cha elimu.
Kwa upande wao, viongozi wa shule pamoja na wananchi walitoa shukrani kwa Benki ya CRDB kwa msaada huo, wakieleza kuwa madawati hayo yataongeza ari ya wanafunzi kujifunza na kuboresha mazingira ya utoaji wa elimu katika shule hizo.
Kampeni ya CRDB-Keti Jifunze ni sehemu ya programu za uwajibikaji kwa jamii zinazotekelezwa na Benki ya CRDB kwa lengo la kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuboresha sekta ya elimu na kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya kujifunzia nchini.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, akikabidhi madawati katika Shule ya Msingi Nguvu Kazi iliyopo Runzewe, mkoani Geita
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa shule pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Nguvu Kazi iliyopo Runzewe, mkoani Geita, wakiwa wamekaa kwenye madawati yaliyotolewa na Benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya juhudi zake za kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuendelea kuwekeza katika sekta ya elimu nchini.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi, Jumanne Wagana, akizungumza na wanafunzi, walimu na wananchi katika Shule ya Msingi Nguvu Kazi iliyopo Runzewe, mkoani Geita, wakati wa hafla ya kukabidhi madawati yaliyotolewa na Benki ya CRDB ikiwa ni sehemu ya mchango wake katika kuboresha mazingira ya kujifunzia na kuendelea kuwekeza katika sekta ya elimu nchini.



































Social Plugin