Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAKEMEA SIASA ZA CHUKI,KATAMBI AWAJIBU WAPINZANI



Na Mwandishi wetu

Waziri wa Mambo ya Ndani ya ,Patrobas Katambi amewahakikishia amani na utulivu wananchi wa Tanzania huku akiwataka kuendelea na shughuli za kiuchumi na maendeleo hata katika tarehe inayotajwa mitandaoni kuwa kutakua na maandamano nchi nzima ambapo amesema Vyombo vya Usalama vimejipanga kulinda amani ya nchi hii ambapo pia ameziomba mamlaka husika kupitia Wakurugenzi wa Miji na Mikoa kusimamia miundombinu ya barabara ili huduma za Uokoaji na zimamoto ziweze kufika katika eneo la tukio.

Amesema hayo wakati wa Hafla ya kufunga Mafunzo ya Awali,Kozi Na.6/2026 katika Chuo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Chogo,kilichopo wilayani Handeni mkoani Tanga ambapo askari 1000 wamehitimu mafunzo hayo.

Akizungumza katika Hafla hiyo Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,John Masunga amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Daktari Samia Suruhu Hassan kwa kutoa kibali hicho cha kuajiri askari hao Elfu Moja huku akithibitisha taratibu zote za ajira kukamilika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com