Na Sumai Salum- Kishapu
Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkoani shinyanga imepokea Mpango Kazi wa Jamii wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (L-CAP) utakaotekelezwa katika Kata 10 kati ya 29 za Halmashauri hiyo kupitia Programu ya Kuwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (Scaling -up Locally Led Climate Action Program - SCALE), inayofadhiliwa na Benki ya Dunia kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka wa fedha 2025/2026 hadi 2029/2030.
Akiwasilisha mpango huo katika kikao maalum cha Baraza la kupokea mpango kazi huo kilichofanyika Juni 26, 2026, katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mratibu wa Programu ya SCALE, Revosatus Mboya, amesema programu hiyo inalenga kuongeza uwezo wa serikali za mitaa na jamii kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi kupitia utekelezaji wa miradi inayotokana na mahitaji halisi ya wananchi.
Amesema Halmashauri imepokea hadi sasa jumla ya TSh milioni 74,496,045.70 kutoka Benki ya Dunia, fedha ambazo zimetumika katika kutambua fursa na vikwazo vya maendeleo, kufanya tathmini shirikishi ya athari za mabadiliko ya tabianchi (PCRA) na kuandaa Mpango Kazi wa Jamii wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (L-CAP).
Mboya amesema Kata zitakazonufaika na utekelezaji wa programu hiyo ni Masanga, Mwamalasa, Somagedi, Shagihilu, Ndoleleji, Lagana, Ngofila, Kiloleli, Mwaweja na Mwakipoya.
Amefafanua kuwa vipaumbele vilivyoainishwa na wananchi ni pamoja na uchimbaji wa malambo ya kuhifadhi maji, uchimbaji wa visima virefu, ujenzi wa miundombinu ya uvunaji wa maji ya mvua, uboreshaji wa kingo za mito na kudhibiti mafuriko, ujenzi wa mitaro ya umwagiliaji, matengenezo ya barabara, upandaji wa miti ya kivuli na matunda, pamoja na ununuzi wa mashine za kutengeneza mkaa mbadala kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Aidha, amesema programu hiyo itatekeleza shughuli za ufugaji wa nyuki kupitia vikundi, ununuzi na usambazaji wa mbegu za mazao yanayostahimili ukame, kuimarisha huduma za ugani pamoja na utoaji wa madume ya borani kwa wafugaji ili kuongeza uzalishaji na kuimarisha ustahimilivu wa jamii dhidi ya athari za mabadiliko ya tabianchi.
Kwa upande wao, madiwani wa Kata zinazonufaika na zisizo na program hiyo wameipongeza Serikali kwa kuileta Programu ya SCALE wakisema miradi iliyopangwa imetokana na maoni ya wananchi na itasaidia kuboresha upatikanaji wa maji, kuimarisha miundombinu, kuongeza uzalishaji wa kilimo na mifugo pamoja na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi katika maeneo yao.
Baada ya mjadala, Baraza la Hilo maalum limepokea na kupitisha Mpango Kazi wa Jamii wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (L-CAP), likielekeza kuendelea kwa utekelezaji wa miradi hiyo kwa ushirikishwaji wa wananchi ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Mratibu wa Programu ya SCALE Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Revosatus Mboya akizungumza kwenye kikao maalum cha Baraza la kupokea Mpango Kazi wa Jamii wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (L-CAP) kupitia Programu ya Kuwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (Scaling -up Locally Led Climate Action Program - SCALE) kilichofanyika Juni 26, 2026, katika ukumbi wa Halmashauri
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Josephat Limbe akizungumza kwenye kikao maalum cha Baraza la kupokea Mpango Kazi wa Jamii wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (L-CAP) kupitia Programu ya Kuwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (Scaling -up Locally Led Climate Action Program - SCALE) kilichofanyika Juni 26, 2026, katika ukumbi wa Halmashauri 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson akizungumza kwenye kikao maalum cha Baraza la kupokea Mpango Kazi wa Jamii wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (L-CAP) kupitia Programu ya Kuwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (Scaling -up Locally Led Climate Action Program - SCALE) kilichofanyika Juni 26, 2026, katika ukumbi wa Halmashauri


Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akizungumza kwenye kikao maalum cha Baraza la kupokea Mpango Kazi wa Jamii wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (L-CAP) kupitia Programu ya Kuwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (Scaling -up Locally Led Climate Action Program - SCALE) kilichofanyika Juni 26, 2026, katika ukumbi wa Halmashauri
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Enock Reuben akizungumza kwenye kikao maalum cha Baraza la kupokea Mpango Kazi wa Jamii wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (L-CAP) kupitia Programu ya Kuwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (Scaling -up Locally Led Climate Action Program - SCALE) kilichofanyika Juni 26, 2026, katika ukumbi wa Halmashauri
Diwani wa Kata ya Mwaweja wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Bujiku Mganga
Diwani wa Kata ya Somagedi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Tabitha Sadikieli
















































































Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Peter Masindi akizungumza kwenye kikao maalum cha Baraza la kupokea Mpango Kazi wa Jamii wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (L-CAP) kupitia Programu ya Kuwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (Scaling -up Locally Led Climate Action Program - SCALE) kilichofanyika Juni 26, 2026, katika ukumbi wa Halmashauri
Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga Mhe. Enock Reuben akizungumza kwenye kikao maalum cha Baraza la kupokea Mpango Kazi wa Jamii wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (L-CAP) kupitia Programu ya Kuwezesha Mamlaka za Serikali za Mitaa Kukabiliana na Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (Scaling -up Locally Led Climate Action Program - SCALE) kilichofanyika Juni 26, 2026, katika ukumbi wa Halmashauri
Social Plugin