Na mwandishi wetu,Arusha
Jeshi la Polisi Mkoani Arusha Jumapili Juni 14, 2026 limekanusha taarifa iliyosambazwa katika Mitandao ya Kijamii Nchini na Mwanaharakati Maria Sarungi, akichapisha picha mjongeo na kudai kuwa yupo Askari Polisi mmoja aliyevamiwa na kupigwa na wananchi katika Moja ya maeneo ya Mkoa wa Arusha.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Justine Masejo katika taarifa yake, amewaambia waandishi wa habari kuwa taarifa hizo ni za uongo, kwani kwa Mkoa wa Arusha hakuna tukio lolote lenye kuhusisha Askari Polisi kupigwa, akisisitiza kuwa hata Video inayosambaza na mtumiaji huyo wa Mitandao ya Kijamii imechukuliwa nje ya Nchi na kisha kutengenezewa maneno ya uongo yenye kuhusisha video hiyo na Mkoa wa Arusha.
"Tunaowamba wananchi kupuuza taarifa hiyo kwa kuwa mtu huyo (Maria) amekuwa akiandaa na kusambaza maudhui ya uongo, uchonganishi na kutaka kuleta taharuki kwa jamii jambo ambalo ni kinyume na makuzi, mila, desturi na mifumo ya kisheria." Amesema Kamanda Masejo.
Polisi ya Arusha kadhalika imetoa wito na onyo kwa baadhi ya watu wenye tabia kama hizo za kuandaa na kusambaza taarifa za uongo, kupandikiza chuki na kuchonganisha jamii, Kamanda Masejo akiwataka kuacha kufanya hivyo kwani ni kinyume cha sheria na taratibu za Nchi.

Social Plugin