Na mwandishi wetu

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Taifa, Mary Pius Chatanda (MCC), leo Juni 6, 2026 amefika nyumbani kwa Mkuu wa Mkoa Mstaafu wa Mwanza, Ndg. Steven Mashishanga eneo la Nyasaka, jijini Mwanza, kutoa pole na faraja kufuatia msiba wa binti yao, Loyce S. Mashishanga.

Binti huyo alifariki dunia Juni 2, 2026 katika Hospitali ya Hindu Mandal, Mwanza Hindu Mandal Hospital, baada ya kuugua.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo ya faraja, Chatanda amewasilisha salamu za pole kwa niaba ya Jumuiya ya Umoja wa Wanawake wa CCM pamoja na Chama Cha Mapinduzi kwa ujumla, akisisitiza mshikamano na familia katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Ameomba Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, na kuipatia familia uvumilivu, nguvu na subira ya kustahimili pigo hilo kubwa la kifamilia.

_“Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea. Mwenyezi Mungu awape faraja na amani katika kipindi hiki cha huzuni,” imesema sehemu ya ujumbe huo wa rambirambi.