Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda ( wa pili kulia), akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakikata utepe kuzindua rasmi Kituo cha Utalii Ikolojia katika Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, akipatiwa maelezo kuhusu shughuli za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) alipotembelea banda la taasisi hiyo wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Utalii Ikolojia katika Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga.
Wasanii wa kikundi cha ngoma ya asili ya Kisukuma cha Wagonyangi wakitumbuiza kwa maonesho ya utamaduni, yakiwemo ya kucheza na nyoka, yaliyovutia wageni na washiriki wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Utalii Ikolojia katika Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua na kutembelea vivutio vilivyopo katika Kituo cha Utalii Ikolojia cha Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga, wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo hicho.
Na Kadama Malunde – Malunde 1 Blog
Shinyanga imepiga hatua mpya katika kukuza utalii wa mazingira baada ya kuzinduliwa rasmi Kituo cha Utalii Ikolojia (Ecotourism) katika Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, mradi unaotarajiwa kuifanya hifadhi hiyo kuwa kivutio kipya cha utalii wa ndani, kuongeza ajira, kuimarisha uhifadhi wa mazingira na kuchochea uchumi wa wananchi kupitia matumizi endelevu ya rasilimali za misitu.
Uzinduzi huo umefanyika leo Juni 27, 2026 katika Msitu wa Hifadhi wa Lubaga uliopo Manispaa ya Shinyanga, ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi wa Serikali, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), wadau wa uhifadhi, sekta ya utalii pamoja na wananchi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Nkinda amesema tukio hilo si uzinduzi wa eneo la utalii pekee, bali ni hatua ya kuonyesha namna ambavyo rasilimali za asili zinaweza kubadilishwa kuwa fursa za maendeleo ya kiuchumi, ajira, elimu na burudani kwa jamii.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, na viongozi mbalimbali wakifanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Msitu wa Hifadhi wa Lubaga na kujionea vivutio vya Utalii Ikolojia vilivyoanzishwa katika hifadhi hiyo.
Amesema kwa muda mrefu watu wengi wamekuwa wakihusisha utalii na mbuga za wanyama, milima na fukwe za bahari, lakini Msitu wa Hifadhi wa Lubaga unaonyesha kuwa hata Shinyanga ina hazina kubwa ya utalii wa mazingira inayostahili kutambulika, kuendelezwa na kutembelewa.
"Mkoa wa Shinyanga unaendelea kupiga hatua katika kuendeleza utalii wa ndani kwa kutumia rasilimali zilizopo. Hii ni fursa muhimu kwa wananchi wetu kujifunza kuwa utalii haupo mbali; unaweza kuanzia hapa hapa nyumbani kwetu," amesema Nkinda.
Amesema utalii wa ndani una mchango mkubwa katika kuongeza mapato ya Serikali, kuibua fursa za biashara kwa jamii, kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na kuimarisha utamaduni wa kuthamini urithi wa asili.
Nkinda amewataka wananchi, shule, vyuo, taasisi, makampuni na familia kutumia Msitu wa Lubaga kwa shughuli za elimu, mapumziko na burudani, akisisitiza kuwa maeneo ya asili yanasaidia pia kupunguza msongo wa mawazo na kujenga afya ya mwili na akili.
Aidha, amewahimiza vijana kutumia fursa zinazotokana na utalii wa mazingira kujiajiri kupitia huduma za wageni, biashara ndogo ndogo, ufugaji wa nyuki na shughuli nyingine zinazohusiana na uhifadhi wa mazingira.
Kwa upande wake, Mhifadhi Mwandamizi wa Misitu TFS Wilaya ya Shinyanga, Fabian Balele, akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli za uhifadhi na utalii ikolojia katika Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga, amesema kituo hicho kimejengwa kwa kuzingatia misingi ya uhifadhi, ambapo hakuna mti uliokatwa wakati wa utekelezaji wa mradi huo, kwani miundombinu yote imewekwa katika maeneo yasiyoharibu mfumo wa ikolojia wa msitu.

Balele amesema kituo hicho tayari kinatoa huduma mbalimbali za utalii ikiwemo utalii wa baiskeli, matembezi ya misituni, maeneo maalumu ya kupiga picha, ukumbi wa mikutano, maeneo ya kupiga kambi (Camping Sites), maeneo ya picnic pamoja na eneo maalumu la Special Moments Corner kwa shughuli kama engagements na matukio mengine ya kijamii.
Ameongeza kuwa ndani ya msitu huo pia kuna shughuli za ufugaji wa nyuki zinazowezesha wageni kujifunza kuhusu Utalii wa Nyuki (Apitourism), sambamba na elimu ya uhifadhi wa mazingira, utunzaji wa miti na mimea tiba.
"Tumehakikisha maendeleo haya yanaenda sambamba na uhifadhi wa mazingira. Hakuna mti uliokatwa kwa ajili ya mradi huu na tunaendelea kuboresha eneo hili kwa kuongeza vivutio mbalimbali vitakavyovutia watalii wengi zaidi," amesema Balele.
Amesema TFS inaendelea na mipango ya kupanua kituo hicho kwa kujenga mabwawa ya kuogelea (Swimming Pools), bustani ya wanyama, viwanja vya michezo kama mpira wa kikapu, mpira wa pete na mpira wa wavu, ukumbi mkubwa wa shughuli mbalimbali, eneo la mazoezi (Gym) pamoja na michezo ya watoto ili kukifanya Lubaga kuwa kitovu cha utalii wa mazingira katika Kanda ya Ziwa.
Mwakilishi wa Kamanda wa TFS Kanda ya Magharibi, Aloyce Kilemwa amefafanua kuwa mradi huo unalenga kuongeza thamani ya misitu ya hifadhi kupitia utalii wa mazingira unaotekelezwa kwa njia endelevu, huku ukihakikisha uhifadhi wa mazingira unaendelea kupewa kipaumbele.
Amesema kupitia utalii huo, jamii na Serikali zitanufaika kiuchumi sambamba na kulindwa kwa mfumo wa ikolojia wa Msitu wa Lubaga kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Naye Mwakilishi wa Meya wa Manispaa ya Shinyanga na Diwani wa Kata ya Ngokolo, Jackline Isaro, amesema uzinduzi wa Kituo cha Utalii Ikolojia cha Lubaga ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia kampeni ya Royal Tour, ambayo imeendelea kuitangaza Tanzania kimataifa kama nchi yenye vivutio vya kipekee vya utalii.
Amesema Manispaa ya Shinyanga itaendelea kushirikiana na TFS kutangaza kivutio hicho ili kuongeza idadi ya watalii na kuhakikisha wananchi wanapata manufaa ya kiuchumi yanayotokana na sekta ya utalii.
Uzinduzi wa Kituo cha Utalii Ikolojia cha Lubaga unatarajiwa kuongeza mchango wa Mkoa wa Shinyanga katika sekta ya utalii nchini, kuchochea biashara zinazozunguka eneo hilo na kuimarisha ushiriki wa wananchi katika kulinda misitu kama urithi muhimu kwa maendeleo endelevu.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda (wa pili kulia), akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wakikata utepe kuzindua rasmi Kituo cha Utalii Ikolojia katika Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, na viongozi mbalimbali wakifanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Msitu wa Hifadhi wa Lubaga na kujionea vivutio vya Utalii Ikolojia vilivyoanzishwa katika hifadhi hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Kituo cha Utalii Ikolojia katika Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Manispaa ya Shinyanga, leo Juni 27, 2026.

Mhifadhi Mwandamizi wa Misitu TFS Wilaya ya Shinyanga, Fabian Balele, akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli za uhifadhi na utalii ikolojia katika Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga.

Mwakilishi wa Kamanda wa TFS Kanda ya Magharibi, Aloyce Kilemwa, akizungumza wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Utalii Ikolojia cha Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga.
Mwakilishi wa Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Jackline Isaro, akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Kituo cha Utalii Ikolojia katika Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Manispaa ya Shinyanga.
Kamanda wa TFS Mkoa wa Shinyanga, Fabian Balele, akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Utalii Ikolojia wakati wa uzinduzi rasmi wa Kituo cha Utalii Ikolojia katika Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua na kutembelea vivutio vilivyopo katika Kituo cha Utalii Ikolojia cha Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga, wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua na kutembelea vivutio vilivyopo katika Kituo cha Utalii Ikolojia cha Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga, wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua na kutembelea vivutio vilivyopo katika Kituo cha Utalii Ikolojia cha Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga, wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua na kutembelea vivutio vilivyopo katika Kituo cha Utalii Ikolojia cha Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga, wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua na kutembelea vivutio vilivyopo katika Kituo cha Utalii Ikolojia cha Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga, wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua na kutembelea vivutio vilivyopo katika Kituo cha Utalii Ikolojia cha Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga, wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua na kutembelea vivutio vilivyopo katika Kituo cha Utalii Ikolojia cha Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga, wakati wa uzinduzi rasmi wa kituo hicho.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, na viongozi mbalimbali wakifanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Msitu wa Hifadhi wa Lubaga na kujionea vivutio vya Utalii Ikolojia vilivyoanzishwa katika hifadhi hiyo,
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, na viongozi mbalimbali wakifanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Msitu wa Hifadhi wa Lubaga na kujionea vivutio vya Utalii Ikolojia vilivyoanzishwa katika hifadhi hiyo,
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, na viongozi mbalimbali wakifanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Msitu wa Hifadhi wa Lubaga na kujionea vivutio vya Utalii Ikolojia vilivyoanzishwa katika hifadhi hiyo,
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, na viongozi mbalimbali wakifanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Msitu wa Hifadhi wa Lubaga na kujionea vivutio vya Utalii Ikolojia vilivyoanzishwa katika hifadhi hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, na viongozi mbalimbali wakifanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali ya Msitu wa Hifadhi wa Lubaga na kujionea vivutio vya Utalii Ikolojia vilivyoanzishwa katika hifadhi hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, akipatiwa maelezo kuhusu shughuli za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) alipotembelea banda la taasisi hiyo wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Utalii Ikolojia katika Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda, akipatiwa maelezo kuhusu shughuli za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) alipotembelea banda la taasisi hiyo wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Utalii Ikolojia katika Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga.
Wafanyakazi wa TFS wakionesha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wakala huo kupitia shughuli za uhifadhi wa misitu na matumizi endelevu ya rasilimali za misitu wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Utalii Ikolojia cha Lubaga, Shinyanga.
Wafanyakazi wa TFS wakionesha bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na wakala huo kupitia shughuli za uhifadhi wa misitu na matumizi endelevu ya rasilimali za misitu wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Utalii Ikolojia cha Lubaga, Shinyanga.
Wasanii wa kikundi cha ngoma ya asili ya Kisukuma cha Wagonyangi wakitumbuiza kwa maonesho ya utamaduni, yakiwemo ya kucheza na nyoka, yaliyovutia wageni na washiriki wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Utalii Ikolojia katika Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga.

Vijana wa sarakasi wakionesha umahiri wao kupitia maonesho ya kuvutia yaliyowaburudisha wageni na washiriki wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Utalii Ikolojia katika Msitu wa Hifadhi wa Lubaga, Shinyanga.

MC Mr Black akizungumza na kuongoza ratiba ya hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Utalii Ikolojia katika Msitu wa Lubaga, Shinyanga.

Social Plugin