Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TANZANIA KINARA WA MIKAKATI YA UHAMIAJI AFRIKA MASHARIKI



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Patrobass Katambi amesema Tanzania imejipanga kikamilifu na Mwelekeo wa sasa wa Uhamiaji Kimataifa unaotokana na Mabadiliko ya misururu ya uhamiaji kutokana na migogoro, mabadiliko ya tabianchi, na hali ya uchumi.

Ameyasema hayo wakati wa kikao cha Jukwaa la Kimataifa la Uhamiaji(International Immigration Review Forum,2026),kilichofanyika New York,Marekani.

Amesema mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na Idadi ya wakimbizi na wahamiaji wa kibiashara, Sera na Sheria za Uhamiaji, Ulinganifu wa sera za nchi tofauti,Athari za mabadiliko ya sheria za uhamiaji kwa usalama wa nchi na huru kwa wakimbizi,Uhakika na Haki za Binadamu,Haki za kisheria na kibinadamu kwa wahamiaji,Njia za kuhakikisha haki za kimsingi kwa wakimbizi na wahamiaji bila nyaraka,Athari za Uchumi na Kijamii

Jinsi uhamiaji unavyowezesha ukuaji wa uchumi, ukosefu wa ajira, au ushindani wa rasilimali na mwingiliano wa wahamiaji katika jamii na soko la kazi.

Katambi amesema pia teeknolojia itumike kuleta Usalama wa Uhamiaji, Kutumia data kubwa (big data) na AI kufuatilia uhamiaji haramu,kulinda faragha na ulinzi wa taarifa binafsi pia kujipanga na Uhamiaji haramu na Mabadiliko ya Tabianchi na

Ushirikiano wa kimataifa na njia za kuboresha ushirikiano kati ya nchi za asili na za marudio kwa upana pia tumejadili maswala ya Kuimarisha masharti ya usafirishaji wa kisheria na utekelezaji wa mkataba wa kimataifa.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com