Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWILI WA VICTORY SENGE KUPOKELEWA LEO SHINYANGA MJINI, MAZISHI JUMATANO BUSHUSHU



Mazishi ya marehemu Victory Emmanuel Senge yanatarajiwa kufanyika Jumatano, Mei 6, 2026 Mjini Shinyanga, kufuatia kifo chake kilichotokea Jumamosi, Mei 2, 2026 katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, jijini Mwanza, alikokuwa akipatiwa matibabu baada ya kukumbwa na changamoto za uzazi.

Marehemu Victory alikuwa Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, ambapo alihudumu kwa weledi na kujenga mahusiano mazuri na wateja pamoja na jamii. 

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Lazaro Jacob Twange.

Mbali na utumishi wake serikalini, pia alikuwa mfanyabiashara aliyefanikiwa na mmiliki wa maduka ya nguo ya Victorious yaliyopo Ngokolo Mjini Shinyanga. 

Kifo chake kimeacha simanzi kubwa kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, wafanyakazi wenzake pamoja na wakazi wa Shinyanga waliomfahamu na kuguswa na mchango wake.

Kwa sasa msiba upo katika eneo la Bushushu, Mwalugoye Mjini Shinyanga, ambapo ndugu, jamaa na marafiki wanaendelea kutoa pole na kushiriki shughuli za maombolezo.

Kwa mujibu wa ratiba ya mazishi, mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili Shinyanga Mei 5,2026 na kupokelewa rasmi kabla ya kupelekwa nyumbani Mwalugoye kwa ajili ya ibada na kuaga mwili.

 Siku ya mazishi, shughuli zitaanza Mei 6,2026 asubuhi kwa ibada ya nyumbani, ikifuatiwa na ibada kanisa la TAG PCC Bushushu. Baadaye, mwili utasindikizwa kwenda makaburini Bushushu (Barabara ya Shy Park) kwa maziko.

Marehemu Victory atakumbukwa kwa uchapakazi wake, moyo wa kujituma na mchango wake katika jamii.

R.I.P Vicky 🕊️
Victory Senge enzi za uhai wake

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com