


Kampuni ya MATI Super Brands LTD yenye makao yake mjini Babati mkoani Manyara, ambayo ni kampuni mama ya MATI Foundation, MATI Zoo na MATI LTD South Africa, imeweka historia kwa kuvunja rekodi ya ushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani mwaka 2026 yaliyofanyika Mei Mosi 2026 katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati, ngazi ya Mkoa wa Manyara, baada ya kuingia na msafara mkubwa wa magari uliovutia hisia za wengi.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga.
@malundeblog  MATI Brands LTD Yavunja Rekodi ya Ushiriki Siku ya Wafanyakazi Manyara , Mulokozi asema 'Tanzania ni Mahali Salama kwa Uwekezaji' Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog Kampuni ya MATI Brands LTD yenye makao yake mjini Babati mkoani Manyara, ambayo ni kampuni mama ya MATI Foundation, MATI Zoo na MATI LTD South Africa, leo Mei Mosi 2026 imeweka historia kwa kuvunja rekodi ya ushiriki katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati, ngazi ya Mkoa wa Manyara. Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mheshimiwa Queen Sendiga. MATI BRANDS LTD ni wazalishaji wa vinywaji changamshi vya aina mbalimbali ikiwemo Strong, Sed na bidhaa nyingine zinazokubalika sokoni. Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa MATI, Bw. David Mulokozi, ambaye ni mwekezaji wa ndani mzawa, amesema Tanzania ni eneo huru, lenye amani na salama kwa uwekezaji wa ndani na nje ya nchi. Amesema mazingira mazuri ya biashara pamoja na fursa nyingi za kiuchumi yaliyopo nchini yanaendelea kuwavutia wawekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda, utalii, kilimo na huduma. Bw. Mulokozi ameweka bayana dhamira yake ya kuendelea kukuza uchumi wa Tanzania kupitia sekta za viwanda, utalii na hifadhi ya mazingira, huku akiwahamasisha wawekezaji wengine kutumia fursa zilizopo nchini kwa maendeleo ya taifa. Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Queen Sendiga amewapongeza wawekezaji wa mkoa huo, akisema Mati Brands LTD ni mfano wa mwekezaji mzuri kutokana na mchango wake kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Amesema kampuni hiyo imesaidia upatikanaji wa ajira kwa wananchi kwa kufungua nafasi nyingi za kazi, pamoja na kushiriki katika huduma za kijamii na kusaidia jamii inayowazunguka. “Niwatie moyo wawekezaji wote wa Mkoa wa Manyara kwamba serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji ili kuinua uchumi wa wananchi. Mati Brands LTD wamekuwa wawekezaji wazuri katika mkoa wetu. Nimeona magari mengi kwenye maandamano na wafanyakazi wengi ambao wamepata ajira katika kampuni hii,” amesema. Aidha, alisisitiza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na wawekezaji wenye nia njema ili kuchochea maendeleo ya Tanzania kwa ujumla. Kwa sasa, MATI BRANDS LTD ni mwajiri wa wafanyakazi zaidi ya 1,000 nchini Tanzania pamoja na ukanda wa nchi za Maziwa Makuu na Afrika Kusini. Sambamba na maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa Vyombo vya Habari na Siku ya Wafanyakazi Duniani, Bw. David Mulokozi na kampuni yake ya MATI BRANDS LTD wameonesha mshikamano na vyombo vya habari kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Vijijini (RUJAT) ili kuhakikisha habari za vijijini pamoja na sauti za pembezoni zinapewa kipaumbele katika vyombo vya habari nchini Tanzania.
♬ original sound - Malunde
@malundeblog Kampuni ya MATI SUPER BRAND inayozalisha Vinywaji Changamshi iliyopo Mkoani Manyara inavyoshiriki Maadhimisho ya MEI MOSI 2026
♬ Brand Promotion - Jim Rocks


































































































Social Plugin