Polisi Kata wa Solwa mkoani Shinyanga, Paul Mashimba, amebainisha kuwa kuwaweka vijana bize na michezo kupitia mashindano ya Niachekona Cup 2026 ndiyo njia salama na endelevu ya kutokomeza uhalifu kuanzia ngazi ya chini.
Alieleza kuwa kijana anapokuwa uwanjani akicheza au kushabikia soka, anakosa kabisa muda na nafasi ya kuwaza matendo mabaya kama wizi, uvunjaji, na matumizi ya dawa za kulevya, jambo linalofanya michezo kuwa nguzo imara inayohakikisha nchi inabaki katika hali ya amani, utulivu, na usalama.
Jeshi la Polisi limepongeza kwa dhati juhudi za muasisi wa ligi hiyo, Paul Daud Augustino, kwa kushirikiana na shirika la Lushu Foundation, likisisitiza kuwa mashindano hayo yanatambulika rasmi kisheria kuanzia ngazi ya kijiji hadi Baraza la Michezo la Mkoa.
Ili kulinda amani hiyo inayojengwa na michezo, Mashimba alitoa onyo kali kuwa sheria itachukua mkondo wake na kuwafikisha mahakamani watu wachache watakaobainika kujihusisha na fujo au uvunjifu wa amani wakati wote , huku akiwasihi vijana kuutumia mshikamano huo kama fursa ya kuibua vipaji na kujenga urafiki.
Social Plugin