Na mwandishi wetu,Dar
Waziri wa Nchi ofisi ya RAIS , Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka amesema tatizo la vijana ni zaidi ya fedha, hivyo wanapaswa kujiandaa ipasavyo kuweza kuzikabili na kuzimudu fursa zilizopo.
Nanauka ameeleza hayo leo , Jumamosi Mei 16,2926 katika kongamano la wanafunzi wa vyuo lenye kauli mbiu 'never again' tuipende, tuitunze , tuilinde nchi yetu' lililofanyika ukumbi wa Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam na kuandaliwa na Jumuiya ya Wanafunzi Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO) mkoani hapa.
Uthibitisho wa hilo, Waziri Nanauka amesema katika wizarani kwake kuna Sh3.9 bilioni ambazo ziko kwenye mikono ya vijana na bado hawajazirudisha.
Tatizo alilobaini kuwa si wizarani pekee bali hata katika halmashauri kuna changamoto kama hiyo ya vijana kutorudisha fedha za mikopo.
“Kwa hiyo tatizo la vijana ni zaidi ya fedha ndio maana sera ya vijana haihusishi kitu kimoja, inazungumza mambo mbalimbali yatakayomfanya huyu kijana kuwa kijana aliyekamilika,” amesema.
Pamoja na uwezeshaji unaofanywa na Serikali Waziri Nanauka amesema kuna haja kwa vijana kujiandaa katika namna ambayo wanaweza wakanufaika na fursa zinazotolewa.


Social Plugin