Nchi waandaji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika mwaka 2027 (AFCON 2027) wamesaini hati ya makubaliano ya pamoja inayojulikana kama CAF Joint Resolution – TotalEnergies AFCON PAMOJA 2027 tarehe 11 Mei, 2026.
Nchi hizo ambazo ni Tanzania Kenya na Uganda zimesaini hati hiyo kwa lengo la kuimarisha uratibu na ushirikiano katika maandalizi ya mashindano hayo makubwa ya bara la Afrika.
Makubaliano hayo yameshuhudiwa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Dkt. Patrice Motssepe
Tanzania imewakilishwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Paul Makonda na Viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakiongozwa na Rais Wallace Karia.

Social Plugin