Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ELIMU YAPEWA KIPAUMBELE: WIZARA YAOMBA TRILIONI 2.39 KUTEKELEZA AJENDA YA 2026/27


Na Dotto Kwilasa, Dodoma

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeomba kuidhinishiwa jumla ya Sh trilioni 2.39 kwa mwaka wa fedha 2026/2027 kwa ajili ya kutekeleza vipaumbele vitano vya sekta hiyo muhimu nchini.

Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo bungeni leo Mei 7, 2026, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Adolf Mkenda amesema kati ya fedha hizo, Sh bilioni 697.84 zimetengwa kwa matumizi ya kawaida.

Profesa Mkenda amesema ndani ya fedha hizo, Sh bilioni 648.08 zitatumika kulipa mishahara ya watumishi huku Sh bilioni 49.75 zikielekezwa kwenye matumizi mengineyo.

Aidha, amesema Wizara hiyo imepanga kutumia Sh trilioni 1.69 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ambapo Sh trilioni 1.33 ni fedha za ndani na Sh bilioni 359.33 zinatarajiwa kutoka kwa washirika wa maendeleo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com