NAIBU Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ngwaru Jumanne Maghembe amesisitiza umuhimu wa vijana katika kuleta maendeleo endelevu na mabadiliko chanya kupitia teknolojia, diplomasia na ubunifu katika ngazi ya taifa na kimataifa.
Mhe. Dkt. Maghembe ameyasema hayo leo Mei 18, 2026 wakati akimwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo katika uzinduzi wa Kongamano la Vijana wa Kitanzania chini ya Umoja wa Mataifa la Tanzania International Model United Nations 2026 linalofanyika Zanzibar.
Amesema vijana wanapaswa kutumia elimu, teknolojia na ubunifu kama nyenzo muhimu za kuchangia maendeleo ya jamii na dunia kwa ujumla, huku akiwataka kushiriki kikamilifu katika majukwaa ya kimataifa yanayojenga uwezo wa uongozi na diplomasia.
“Mtumie mkutano huu kubadilishana mawazo, kujenga ushirikiano na kuibua suluhisho za changamoto mbalimbali zikiwemo mabadiliko ya tabianchi, ukosefu wa ajira, usawa wa kijinsia na maendeleo ya teknolojia,” amesema Mhe. Dkt. Maghembe.












Social Plugin