Na mwandishi wetu, Dar
Jengo la Ghorofa Sita lililopo maeneo ya Masaki,jijini Dar es Salaaam limenusurika kuungua moto baada ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuzuia moto uliowaka katika ghorofa ya sita ambapo chumba kimoja na sebule vimeungua huku Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji(Kinondoni),ASF Jacob Chacha akieleza chanzo cha moto kuanzia kwenye eneo la Kiyoyozi.
Akizungumza katika eneo la tukio,Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi ambae alifika eneo la tukio Masaki, akitokea katika ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Mwigulu Nchemba ambapo Waziri Mkuu alitembelea eneo la Soko la Simu 2000,Mawasiliano jijini Dar es Salaam kufuatia ajali ya moto iliyotokea April 4,2026 ambapo uliteketeza vibanda 280 vya wafanyabiashara ndogo ndogo ambapo uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea huku Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifanikiwa kuokoa vibanda 280.
Waziri Katambi amelipongeza Jeshi la Zimamoto kwa kuweza Kudhibiti moto huo kutounguza vibanda 280 katika eneo la mawasiliano sambamba na Kudhibiti moto eneo la Masaki na kuokoa Jengo hilo la ghorofa Sita.

Social Plugin