Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WITO WA UMOJA NA AMANI WATOLEWA, WATANZANIA WAKIISUBIRI RIPOTI YA OKTOBA 29



Watanzania wamehimizwa kupendana, kushirikiana na kudumisha amani, utulivu na mshikamano wakati huu ambapo Serikali inasubiri kukabidhiwa ripoti ya Tume huru ya uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Wito huo umetolewa na Bw. Frank Rungwana, Mkazi wa Kimara Jijini Dar Es Salaam leo Jumanne Aprili 07, 2026, ikiwa ni siku chache tangu kuongezwa siku kwa Tume hiyo ili kuiwezesha Tume kukamilisha uchambuzi wa ushahidi, taarifa na maoni yaliyokusanywa, pamoja na kutoa nafasi kwa wataalamu wa uchunguzi wa kisayansi kuchambua vielelezo vipya vilivyowasilishwa pamoja na kusaidia maandalizi ya ripoti ya mwisho itakayowasilishwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan, ikiwemo tafsiri ya hati hiyo kwa matumizi mapana zaidi.

"Ripoti ya Tume kwanza wengi wasichokijua ni kuwa Tume hii imekuwa huru sana katika kazi zake na kuweka wazi kila ambacho watakibaini. Sisi Watanzania lazima tuachane na propaganda na uzushi wa mitandaoni, tufuatilie, tuchunguze mambo na tuwe na imani na serikali ya Rais Samia.

 Niombe tuwe na subira, tuachane na mambo ya mitandaoni na zaidi wakati huu tunasubiri ripoti niombe tupendane, tuwe na mshikamano na zaidi tukumbuke kuwa tuna Tanzania hii moja tu." Amesema Bw. Rugwana.

Rugwana amesisitiza pia umuhimu wa kutunza amani na kuipa nafasi tume hiyo kuendelea kufanya kazi zake kwa uhuru, badala ya kuwashambulia wajumbe na Viongozi wa Tume hiyo pamoja na kuzungumzia masuala ambayo hayafamiki na kuyahusisha na ripoti hiyo ilihali bado haijakamilika na kukabidhiwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Tume huru ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi Mkuu wa Tanzania ilianza kazi zake Novemba 20, 2025, wananchi na makundi mbalimbali yakishiriki kwa kutoa ushahidi kwa njia ya mahojiano, kutuma ujumbe mfupi wa simu, kuwasiliana kwa njia ya simu na mitandao ya kijamii waliowasiliana kwa njia ya simu hatua iliyosaidia kupanua wigo wa uchunguzi.

Tume hiyo ilipewa jukumu la kubaini chanzo halisi cha matukio yaliyofanyika wakati na baada ya uchaguzi, kujua lengo la walioratibu na kushiriki kufanya vurugu, kuchunguza madhara yaliyojitokeza wakati na baada ya uchaguzi, kuchunguza na kubainisha madhara yaliyojitokeza, kuchunguza mazingira na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na serikali na vyombo vyake, na mtu yeyote au taasisi nyingine katika kubaini na kukabiliana na yaliyotokea sambamba na kupendekeza maeneo yanayohitaji kuimarishwa zaidi ili kuongeza uwajibikaji wa viongozi na raia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com