Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATANZANIA WAASWA DHIDI YA MATUMIZI MABAYA YA MITANDAO YA KIJAMII



Na mwandishi wetu

Wito umetolewa kwa kila Mtanzania kuwa Balozi wa amani kuanzia ngazi ya familia hadi Taifa kwa kukataa kushiriki ama kuhamasisha matendo yoyote yenye harufu ya uvunjifu wa amani ili kuhakikisha Tanzania inaendelea kubakia kuwa kisiwa cha utulivu na mfano wa kuigwa barani Afrika huku ikiendelea kuimarisha mazingira rafiki kwa uwekezaji, ustawi na maendeleo ya kila mmoja.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Aprili 22, 2026 na Bi. Zakhia Mussa Mkazi wa Kiwalani Jijini Dar Es Salaam akibainisha kuwa jamii isiyokuwa na vurugu, mifarakano na mivutano ya kijamii ndiyo jamii ambayo mara zote huzaa Taifa tulivu, lenye amani na usalama na hivyo kutoa nafasi na uhuru kwa kila mmoja kuweza kuendeleza shughuli zake za kiuchumi na kijamii bila ya hofu na wasiwasi.

Zakhia amesisitiza pia umuhimu wa matumizi sahihi ya Mitandao ya kijamii kama daraja la maendeleo badala ya kuyafanya majukwaa hayo kuwa chombo cha kueneza habari za uchochezi na chuki, kila mmoja akihimizwa kujitenga na kukataa taarifa zenye viashiria vya uvunjifu wa amani zinazotokana na uzushi, zikiwa na lengo la kuzua taharuki na kueneza chuki kwa jamii.

Mwananchi huyo amebainisha kuwa matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yanatishia usalama na amani ya Tanzania kwani yanaweza kuchochea chuki za kidini, kikabila au kisiasa ambazo ni hatari kwa umoja na amani iliyopo nchini tangu enzi za waasisi wa Taifa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com