Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

‎WAFANYAKAZI WA TUME YA TAIFA YA MIPANGO WATAKIWA KUWA WABUNIFU NA WELEDI


Katibu Mkuu-Mipango na Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango Dkt Tausi M. Kida ametoa wito kwa watendaji wa Tume hiyo kufanya kazi kwa weledi, ubunifu na ushirikiano ili kuishi dhana ya kufanya kazi isivyokawaida ili kuyafikia matarajio ya Taifa jumuishi, lenye ustawi, haki na linalojitegemea.
‎Dkt. Kida ametoa wito huo leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Tume ya Taifa ya Mipango.
Aidha, amesisitiza ‎kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inayo matarajio makubwa kwa Tume ya kuhakikisha inatekeleza ipasavyo majukumu yake kwa weledi, ari na kuzingatia utu.
‎Mkutano huo, umeongozwa na kauli mbiu isemayo: Utumishi Imara ni Msingi wa Utekelezaji wa Dira 2050.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com