Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TUME YA MATUKIO YA OKTOBA 29 NI HURU NA HAIINGILIWI NA YEYOTE- OTHMAN CHANDE



Mwenyekiti wa Tume huru ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025, Jaji Mstaafu Othman Chande amesisitiza kuwa Tume hiyo inajitegemea kwa kila kitu, akisisitiza kuwa Mamlaka zilizowapa kazi wanakutana tu wakati wa kupewa hadidu za rejea na wakati wa kukabidhi ripoti ya mwisho kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo Jumatano Aprili 08, 2026, Jaji mstaafu Chande amesisitiza kuwa katika hatua ya mwisho pia ya kukamilisha kazi waliyopewa kwa kuchambua ushahidi kwa kina ili kuhakikisha ripoti yao inakuwa na ubora unaotakiwa na kusema itatolewa kwa lugha ya Kiswahili na tafsiri kwa lugha ya Kiingereza.

"Tume inajitegemea kwa kila kitu, Tume ndio mhariri, ndio msahihishaji na mamlaka iliyotupa kazi tunaonana nayo wakati tunapewa hadidu za rejea na wakati tunamkabidhi ripoti ya mwisho. Hakuna mtu yoyote hapa katikati, hatuna dalali, tunafanya kazi yetu tumalizie na tupo katika hatua ya mwisho katika kutafsiri." Amesema Jaji mstaafu Chande.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com