Mwenyekiti wa Bodi wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), David Nchimbi, amesema umefika wakati kwa Watanzania kuingia kikamilifu katika maisha ya kidigitali, akibainisha kuwa shirika hilo limejipanga kutoa huduma mbalimbali za kisasa ikiwemo intaneti ya Faiba.
Nchimbi ametoa kauli hiyo leo Aprili 15 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kituo cha Kijitonyama FTTx Experience Center, ambacho kinalenga kusogeza huduma za kidigitali karibu zaidi na wananchi, hususan majumbani na maofisini.
Amesema matumizi ya teknolojia yatawezesha wananchi kufanya mambo mengi kwa urahisi zaidi, ikiwemo kudhibiti vifaa vya nyumbani kwa kutumia mtandao.
“Tunapaswa kufikia hatua ambayo majumbani mwetu tunaweza kufunga mapazia kwa kutumia mtandao, taa kuwaka usiku na kuzimika mchana kwa mifumo ya kisasa ya kidigitali,” amesema Nchimbi.
Aidha, amesisitiza kuwa huduma hizo zitaboresha maisha ya Watanzania kwa kuwawezesha kupata burudani na huduma nyingine muhimu kwa urahisi wakiwa majumbani mwao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TTCL, Moremi Marwa, amesema huduma ya intaneti ya Faiba itapatikana katika maeneo mbalimbali ikiwemo maofisini, majumbani pamoja na sehemu za wazi kama viwanja na masoko.
Marwa ameongeza kuwa utekelezaji wa mkakati huo tayari umeanza kuzaa matunda, ambapo shirika limeanza kuona ongezeko la mapato na faida ya kifedha tangu kuanza kwa mpango huo mwaka jana.




.jpg)


Social Plugin