
Na Mwandishi wetu - Kahama
Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi ya (CCM) imetoa rai kwa Mkandarasi anayetekeleza ujenzi wa Barabara ya Kahama-Kakola yenye urefu wa Kilomita 73 kwa gharama ya zaidi ya Shilingi bilioni 100 kuongeza kasi ya ujenzi ili kuhakikisha Mradi huo anakamilisha kwa wakati kama mkataba unavyoelekeza.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga, baaada ya kutembelea ujenzi wa Barabara hiyo ambao umefikia asilimia zaidi ya asilimia 70 ya utekelezaji wake amesema kukamilika kwake kutasaidia kukuza Uchumi wa wananchi wa Mikoa ya Shinyanga na Geita.
Amesema CCM katika Ilani yake ya Uchanguzi ya Mwaka 2025/30 inayosimamiwana Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan iliahidi kutekeleza ujenzi wa Barabara hiyo hiyo ni budi Mkandarasi huyo akafanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha anakamilika kama mkataba unavyooelekeza.
“Kamati imeridhika na utekelezaji wa Mradi huu ila ongezeni juhudi tunataka ifikapo Septemba Mwaka huu ukamilike kama mkataba unavyoelekeza,tunaomba na Wale ambao wanamadai yao kuhusu fidia nao walipwe ili ukikamilisha kusiwe na kero,”amesema Myonga.
Awali akitoa taarifa ya Ujenzi wa Barabara hiyo Msimamizi wa ujenzi wa Barabara hiyo Mhandisi John Kalando kutoka TANROADS amesema tayari mkandarasi amekwisha lipwa fedha za ujenzi wa Barabara hiyo na watamsimamia ili ajenge usiku na Mchana ilikwenda na takwa la Mkataba la kamilisha ujenzi huo Septemba Mwaka huu.
Amesema vifaa vyote vya ujenzi katika Mradi huo tayari vimeshafikishwa katika eneo la Mradi hivyo na TANROAD itamsimamia kikamilifu ili kuhakikisha Barabara hiyo inakamilika kwa Wakati na kuleta tija kwa Wakazi wa Mikoa ya Shinyanga na Geita ambao ni Wachimbaji wa Madini na Wakulima.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Msalala Mabula Magangila amesema kamilika kwa Barabara hiyo kutasaidia kuonda adha ya vumbi kwa Wakazi wa Mji ya Segese,Lunguya na Kakola kutokana na Barabara ya awali iliyokuwa na vumbi ila kwa sasa Matumaini yameanza kuonekana.
“Barabara hii ni kiungo muhimu kwa Maendeleo ya Wakazi wa jimbo Msalala,kwa sasa tutakuwa tukisafiri kwa kutumia dakika 45 hadi 50 kufika Kahama tofauti nah apo awali ambapo tulilazimika kutumia saa 5 hadi 6 kwa umbali wa kilomita 75,”amesema Magangila.
Ujenzi wa Barabara hii unatekelezwa kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation kwa gharama ya Shilingi Bilioni 101.2 kwa ufadhili wa Kampuni ya Madini ya Barrick Tanzania Mining Companies (BTMCs) na Serikali ya Tanzania.










Social Plugin