
Benki ya CRDB imejitokeza kuwa mdhamini mkuu wa maonyesho ya mifugo Kanda ya Ziwa ambayo yameandaliwa na kampuni ya FARMFLEX GROUP inayoongozwa na Mkurugenzi Charles Nduku.
Akizungumza na waaandishi wa Habari Mkurugenzi Charles Nduku amesema maonyesho ya mifugo kanda ya ziwa yatakuwa ni makubwa sana na yanaenda kufungua kanda ya ziwa katika ufugaji kibiashara kama ilivyo kauli mbiu ya maonyesho hayo "FUGA KIBIASHARA".
"Maonyesho ya mifugo Kanda ya ziwa yatafanyika tarehe 30 na 31 mwezi Mei 2026 viwanja vya Busanda mkoani Shinyanga lengo ni kuonyesha mifugo na mbegu bora, vilevile kutakuwa na wataalamu wabobezi wa mifugo kutoa elimu, kutakuwa na mbio za baiskeli, Ngoma asili, nyama choma na vyakula vya asili, zitakuwepo taasisi mbali mbali zikiwemo benki kama CRDB Kutoa huduma za kibenki kama akaunti, mikopo na BIMA za mifugo."
Mkurugenzi Charles amewaomba wana Shinyanga, kanda ya Ziwa na Tanzania nzima kujitokeza kwa wingi.
Naye meneja wa CRDB Kanda ya Magharibi yenye makao makuu yake mkoani shinyanga Cpb. Jumanne Wambura Wagana amesema benki ya CRDB ndiyo mdhamini mkuu wa maonyesho hayo ya mifugo ambayo yatafanyika mkoani Shinyanga na CRDB itakuwepo kutoa elimu ya kifedha kwa siku zote mbili.
"Sisi kama benki kiongozi nchini Tanzania na benki inayoongoza kuwawezesha wakulima na wafugaji nchini, ndiyo wazamini wakuu wa maonyesho haya ya mifugo na Ikumbukwe kwamba CRDB ilisaini makubaliano na Chama cha wafugaji Tanzania (CCWT) chini ya mwenyekiti wake Murida Mshota kuwakopesha wafugaji wote nchini mikopo kwa riba nafuu ili wafuge kibiashara, hivo basi tutashiriki pia kwenye maonyesho hayo ili kutoa hamasa kwa wafugaji kutumia huduma za kibenki ikiwemo akaunti ya wakulima na wafugaji isiyo na makato maarufu kama FAHARI KILIMO , Mikopo kwa wafugaji , BIMA ya mifugo na Elimu ya kibenki.








Social Plugin