CEO wa Mara Online, Jacob Mugini (aliyevaa suti), akikabidhi Smart TV kwa walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Manga.
Wanafunzi na walimu wa Shule ya Sekondari Manga wakifurahi kupokea zawadi ya Smart TV kutoka Mara Online, Ijumaa iliyopita.
Na Mwandishi Wetu - Tarime
Mara Online wamekabidhi zawadi ya TV yenye ukubwa wa inchi 55 kwa Shule ya Sekondari Manga iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, mkoani Mara.
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Mara Online, Jacob Mugini, alikabidhi zawadi hiyo kwa walimu na wanafunzi wa shule hiyo Ijumaa iliyopita.
“Tuliahidi kuwapatia zawadi ya TV kama mlivyotuomba na leo tumefurahi kuwaletea Smart TV,” alisema Mugini ambaye pia ni mwandishi wa habari kitaaluma na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Sauti ya Mara na chombo cha habari cha mtandaoni cha Mara Online News.
Kwa upande wake, Mkuu wa Shule ya Sekondari Manga, Mwalimu Editha Nakei, aliishukuru Mara Online kwa ‘Smart TV’ hiyo na kuahidi kwamba itatumika vizuri kwa malengo yaliyokusudiwa.
Manga ni miongoni mwa shule maarufu za serikali katika wilaya ya Tarime, ambayo inapokea wanafunzi wa kike na wavulana kwa kidato cha kwanza hadi cha nne na wanafunzi wa kike pekee kwa kidato cha tano na cha sita.
Mwaka juzi, Mara Online pia walikabidhi zawadi ya TV kwa Shule ya Sekondari JK wakati wa mahafali ya kidato cha nne, ambapo CEO Mugini alipewa heshima ya kuwa mgeni rasmi.



Social Plugin