
Meneja wa Vipindi na Ubunifu kutoka Jambo Media, Renatus Kiluvia maarufu kama Bizzo Fresh, akizungumza na kuelezea maandalizi na umuhimu wa Live Comedy Show itakayofanyika Kahama.

Mchekeshaji Joo Master akizungumza kwa kujiamini kuhusu maandalizi ya wasanii, akieleza namna walivyojipanga kikamilifu kuhakikisha wakazi wa Kahama mkoani Shinyanga wanapata burudani ya vichekesho yenye viwango vya juu.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kampuni ya Lake Talent, kwa kushirikiana na Gakala Health Center, wanakuletea tamasha kubwa la vichekesho litakalotikisa mji wa Kahama, Jumamosi, Aprili 4, 2026, katika Mkesha wa Pasaka, kuanzia saa 1:00 usiku katika Ukumbi wa Malex.
Tamasha hili linatarajiwa kuwakutanisha mastaa mbalimbali wa vichekesho na burudani kutoka ndani na nje ya nchi, kwa usiku mmoja wa kicheko kisicho na kikomo.
Akizungumzia maandalizi ya tukio hilo, Meneja wa Vipindi na Ubunifu kutoka Jambo Media, Renatus Kiluvia maarufu Bizzo Fresh, amesema kila kitu kimekamilika kuhakikisha show hiyo inakuwa ya kipekee na ya kukumbukwa.
“Kahama show kubwa ni moja tu , pale Ukumbi wa Malex! Tumejipanga kuleta burudani ya kiwango cha juu kabisa,” amesema Bizzo Fresh.
Ameongeza kuwa lengo kuu ni kuwakutanisha wakazi wa Kahama na maeneo ya jirani kupitia burudani safi ya vichekesho vyenye ubunifu na mvuto wa hali ya juu.
"Tamasha hili linalenga kutoa burudani kwa wananchi pamoja na kukuza vipaji vya vijana katika tasnia ya vichekesho. Stand-up comedy imekuwa chanzo cha ajira kwa vijana wengi, na sasa imebadilika kutoka uchekeshaji wa kawaida hadi kuwa biashara inayowaingizia kipato. Sisi kama Jambo Media tumeamua kuwaunga mkono vijana hawa,” amesema Kiluvia.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, mchekeshaji Joo Master (Jo Master) amewataka wakazi wa Kahama kujitokeza kwa wingi kushuhudia tamasha hilo, akiahidi burudani ya hali ya juu.
“Tupo Kahama, show ipo, na tumejipanga kikamilifu kuhakikisha kila mtu anacheka bila kikomo,” amesema.
Amesema tamasha hilo litakuwa la kipekee na wasanii wote wako tayari kuwapa mashabiki burudani ya kiwango cha juu, itakayowafanya kuvunja mbavu kwa kicheko.
Jo Master amewahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani hii ya kipekee, akisisitiza kuwa huu ni usiku maalum wa kuondoa msongo wa mawazo na kufurahia maisha kupitia vichekesho vyenye ubunifu na vicheko visivyo na kikomo.
Tamasha hilo litapambwa na mastaa maarufu wakiwemo:
👉 Wanani
👉 Dogo Pepe
👉 MC Ndembo
👉 Shaf Brand
👉 Godfrey Steven
👉 Man Kush (254 Kenya)
👉 Joo Master
Pia, tamasha litashirikisha wachekeshaji chipuzi wakali, wakiwemo MC Ndabitha na Daines, wakiahidi kuwachangamsha mashabiki kwa vichekesho vya kipekee.
🎟️ VIINGILIO:
✨ Platinum: Sh 15,000/- (Mlangoni Sh 20,000/-)
💫 Gold: Sh 50,000/-
🛋️ Sofa Single: Sh 150,000/-
❤️ Sofa Couple: Sh 250,000/-
📍 SEHEMU ZA KUPATIA TIKETI:
🛒 Vunja Bei
📻 Magic 101
🏬 Best Choice Store
👗 Sodox Fashion
💄 JJ Cosmetic
🎬 Kichomi Studio
📲 Pia kupitia Nilipe App
USIKOSE! Kahama inaenda kucheka kwa nguvu – nawe uwe sehemu ya burudani hii kubwa! 😂🔥
📞 MAWASILIANO:
📲 0754 418 189









Social Plugin