Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WABUNGE WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMANI NA TAKUKURU TUHUMA ZA RUSHWA GEITA


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Geita imewafikisha katika mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, wabunge wa majimbo ya Chato Kaskazini na Chato Kusini wakituhumiwa vitendo vya rushwa.

Washitakiwa wengine ni madiwani wanne wa kata tofauti katika Halmashauri ya Wilaya ya Chato, ambao wanadaiwa kushirikiana na wabunge haokupanga na kutekeleza vitendo vya rushwa.


Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Geita, James Ruge ametoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari mjini Geita na kueleza hatua hiyo imefikiwa baada ya uchunguzi wa kina juu ya tuhuma zilizokuwa zinawakabili.


Amewataja watuhumiwa hao ni Mbunge wa Chato Kaskazini, Cornel Magembe na Mbunge wa Chato Kusini, Paschal Lutandula pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chato Diwani wa Kata ya Bwongera, Batholomeo Manunga.


Wengine ni diwani wa Kata ya Mganza, Frank Francis, Diwani wa Kata ya Bwera Josephat Manyenye na Diwani wa Kata ya Muungano Njile Mboligo.


Amesema watuhumiwa wote wamefikishwa Mahakama ya Hakamu Mkazi Geita leo Machi 9, 2026, wakihusishwa na vitendo vya rushwa kwenye mchakato wa uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM)

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com