Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KISA CHA MTOTO NELSA CHAREJEA: MAPENZI YA SIRI, FEDHA ZA MICHANGO NA TASWIRA MITANDAONI


Kisa kilichowahi kugusa mioyo ya Watanzania kinarejea tena mezani, kikichorwa upya na mvutano mpya:Mtoto Nilsa enzi za uhai wake (Mungu amrehemu) akiwa pamoja na Baba yake, Simon Bryson Mnyola wanashughulika na mjadala mkali kuhusu matumizi ya fedha za michango ya watanzania na namna taswira ya mtoto inavyo tumika mitandaoni.


Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Kisa kilichowahi kugusa mioyo ya Watanzania kuhusu mtoto Nilsa, aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kichwa kujaa maji na baadaye kufariki dunia, kimerudi tena katika mjadala wa umma kufuatia kuibuka kwa tuhuma mpya kutoka kwa mama mzazi wa mtoto huyo Jesca.

Kwa mujibu wa maelezo ya mama huyo, aliyewasiliana na chombo hiki kwa njia ya simu, anadai kuwa aliyekuwa mume wake Simon Bryson mnyola (baba nilsa)

alitumia kisa cha mtoto wao kama fursa ya kujipatia fedha kupitia michango ya wananchi, huku akijenga taswira ya kuwa mzazi mwenye upendo mkubwa mitandaoni, jambo ambalo anadai halikuwa halisi.

Jesca anadai kuwa wakati wa ugonjwa wa mtoto, baba huyo alimchukua mtoto na kupiga naye picha ambazo baadaye zilisambazwa mitandaoni kwa lengo la kuibua huruma kwa umma na kuchochea michango ya matibabu.

Kutokana na hali hiyo, Watanzania wengi waliguswa na kuanza kutoa misaada ya fedha.

Hata hivyo, mama huyo anasema baada ya kifo cha mtoto, jumla ya fedha zilizopatikana zilifikia takribani shilingi milioni 17, ambapo anadai alipewa kiasi cha shilingi milioni tatu pekee kwa ajili ya kulipia madeni ya matibabu, huku fedha zilizobaki zikibaki chini ya usimamizi wa baba huyo bila ushirikishwaji wa pamoja.

Aidha, anaeleza kuwa baada ya tukio hilo, mawasiliano kati yao yalivunjika na juhudi zake za kuomba msaada zaidi hazikupata ushirikiano.

Badala yake, anadai kuwa baba huyo ameendelea kutumia jina la mtoto huyo kujitangaza katika shughuli zake za kibiashara mitandaoni.

Katika hatua nyingine, mama huyo anadai kuwa kulikuwa na jitihada za kuonyesha hadharani kuwa wana uhusiano mzuri, ikiwa ni pamoja na kupiga picha pamoja na kuchapishwa mitandaoni, jambo ambalo anasema lilifanyika kwa shinikizo ili kulinda taswira ya baba huyo mbele ya umma.

Wakati huo huo, uchunguzi wa maoni ya mitandaoni unaonyesha kuwepo kwa mgawanyiko wa mitazamo miongoni mwa wananchi, ambapo baadhi wanaendelea kumuunga mkono baba huyo, huku wengine wakianza kuibua maswali kuhusu uwazi wa matumizi ya fedha za michango pamoja na nafasi ya mama mzazi katika mchakato mzima.

Hata hivyo, jitihada za kumpata baba anayehusishwa na tuhuma hizo ili kutoa ufafanuzi wake hazijafanikiwa hadi wakati wa kuchapishwa kwa habari hii.

Hapo chini nimekuwekea baadhi ya maoni ya waliokuwa mashabiki wa Nilsa kwenye mitandao ya kijamii ambapo wengi wameonesha hisia zao moja kwa moja









Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com