
Katibu Mkuu Lukas Mlipu wa TAMESOT (wanne kutoka kushoto) akiwa na viongozi wa wa TAMESOT pamoja waganga mkoa Morogoro

Katibu mkuu wa TAMESOT Lukas na waganga mkoa Katavi
Na Theophilida Felician - Morogoro.
Kufuatia Chama cha Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini (TAMESOT) kuendeleza juhudi za kuhakikisha tiba asili na tiba mbadala inainuka na kupiga hatua chama hicho kimeunda mfumo mpya wa kuwapata viongozi wenye uwezo wa kusimamia shughuli mbalimbali za tiba asili ndani ya chama hicho.
Ametoa kauli hiyo katibu mkuu wa TAMESOT taifa Bw Lukas Joseph Mlipu baada kuhitimisha ziara mikoa kadhaa akilenga kuhamasisha waganga masuala muhimu yahusuyo taaluma hiyo pamoja na kuunda safu mpya ya viongozi ndani ya chama.
Kiongozi huyo ambaye amehitimisha ziara yake kata Mziha wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ameyataja mafanikio ikiwemo ya kuwapata viongozi kuanzia ngazi ya Vijiji, Kata, Wilaya na Mikoa kwa kila mkoa ni viongozi 9 na wilaya 9 huku vijiji na kata wakiwa viongozi 7 na vijiji 7 hivyo vijiji 1105, kata 269, wilaya 40 na mikoa 13 tayari imekamilisha zoezi hilo na kupatika jumla ya viongozi 10095 katika maeneo hayo.
Katibu mkuu Lukas amesema licha ya kuwateua viongozi pia zoezi hilo limekuwa sambamba na kuwapa elimu elekezi viongozi hao ili kuwasaidia kufanya kazi kwa ueledi zaidi.
Amefafanua kuwa ziara hiyo iliyowafikia jumla ya waganga 542 imekuwa na mafanikio pamoja na changamoto ikiwemo ya baadhi ya waratibu wa baraza latiba asili na tiba mbadala katika halmashauri hususani kutotoa ushirikiano ipasavyo jambo ambalo amelitaja kama moja ya sababu yenye kukwamisha malengo na nia njema ya serikali katika kuuthamini na kuutambua mchango mkubwa wa tiba hiyo kwa jamii, ambapo hakusita kuwapongeza waratibu wa halmshauri za Ilemela Mkoa wa Mwanza na Mvomero mkoa wa Morogoro kwa jinsi walivyokuwa naye bega kwa bega katika kuwafikia waganga bila kulisahau Jeshi la polisi mikoa yote ambalo mara kadhaa limekuwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano thabiti kwa kiongozi huyo.
Aidha ameitaja mikoa iliyohusisha zoezi la kuwapata viongozi ni pamoja na Mbeya, Shinyanga, Geita, Mwanza, Mara,Pwani, Tanga, Morogoro, Arusha, Manyara, Kagera na Dare es salaam.
Hata hivyo ameongeza kuwa matarajio ya TAMESOT yenye ofisi zake Kibaigwa Dodoma imeendelea kujitanua zaidi ikiwemo kupata Ardhi yenye ukubwa wa Hekari 100 itakayokuwa eneo mahususi la kupanda mimea ya tiba pamoja na kuchapisha vitabu vya miongozo, kanuni na katiba kwa viongozi na waganga wote kwa ujumla.
Mratibu wa bara za la tiba asili halmshauri ya Mvomero, David Rubadanja amekipongeza chama hicho kwa jinsi kinavyoendesha mambo yake kwakuzingatia mifumo iliyo wazi na yenye kufuata kanuni na taratibu za serikali tofauti na ilivyo kwa vyama vingine.
Ametoa wito kwa waratibu wengine kuuendelea kukiunga mkono chama hicho kutokana na dhamira kiliyonayo yakuyaleta mageuzi ya tiba asili ili iweze kupiga hatua mbele huku akiwasihi waganga kutoa tiba sahihi kwa kufuata misingi ya taaluma hiyo ili kuepukana na dhana potofu ya utapeli.


Social Plugin